Kupitia ukurasa wake wa Facebook ambao anatumia jina la Pancho Magawa Saymon, producer maarufu kwa jina la Pancho Latino wa Bhitz, ameandika kitu ambacho kimeonekana kumkera sana na kwa muda mrefu kinachohusiana na wasanii wanaopenda kwenda ofisini kwake na kutaka kufanyiwa ngoma bure kwa mgongo wa urafiki wao. Haya ndio maneno aliyoyaandika Pancho:
"Hey Guys,Natangaza Rasmi sina urafiki na Msanii yoyote yule.Bhits Ni ofisi kama ofisi zingine so heshima kwanza ifate mkondo wake Then Kwa sababu sina Urafiki na Msanii yoyote inamaana sirecord bure Nimechoka na wasanii wanasumbua kutaka msaada wa kurecord Bure.NOTE-Sirekodi Bure kwa msanii yeyote yule.Ni hayo tu Siku njema#Tokabhitz".
Hii ni tabia ambayo imezoeleka kwa wasanii wengi wa hapa bongo, so Pancho amewakilisha producers wengine pia kuwafikishia ujumbe wasanii kuwa, wanatakiwa kuwathamini waandaji wa muziki kutokana na kwamba kazi wanayoifanya ni kubwa na ambayo inaweza kuyabadili kabisa maisha ya msanii pale inapokuja kuhit na kumpa nafasi msanii kufanya shows nyingi na deals nyingine nyingi. Na ukizingatia producer wa audio analipwa pesa kidogo sana ukilinganisha na director wa music videos zinazofanywa baada ya audio kuwa imetengenezwa.
No comments:
Post a Comment