Game |
The West Coast rapper Game anazidi
kuelekeza bunduki yake yenye risasi za diss kwa Jigga na sasa amekuja kivingine
akimtuhumu kwa kusababisha Obama aperfom chini ya kiwango katika mdahalo
uliopita.
Alipoulizwa mtazamo wake kwa performance ya
Obama katika mdahalo kwake ilikuwa ni
kama alipewa gap la kumsema Jigga, Game aliunganisha tukio la mdahalo wa Obama
na Romney uliofanyika mapema mwezi huu na ushiriki wa Jay-Z katika kampeni za
Obama.
Alifunguka kwa kujiachia, “Nimeona mdahalo:
maneno hayakuwekwa poa saana, baadhi ya mada zilikuwa covered kwa usahihi.”
Baada ya hayo mawazo ya jumla, akafunguka zaidi “lakini alikuwa Obama.
Inawezekana alimsikiliza Jay-Z kabla ya kuingia pale he was a little bit in the
zone and couldn’t get it together. Lakini nampenda Obama ameshapata kura
yangu.”
Baada ya hayo aliamua kuweka msisitizo
alipokuwa anafanya mahojiano na CBS Local “ngoja nikwambie kitu, Obama angeweza
kuja na akasema A-B-C zake katika hiyo debate na bado angepata kura yangu.
Nampenda Obama, ametulia na ana Swag na huyo ndiye rais wangu. Mitt Romney ni
wa Republican. Na siungani na chochote wanachokisimamia. Sio kama na diss imani
ya mtu mwingine yeyote na anachokipigia kura, lakini mimi nampenda Obama. And
he can’t do no wrong.” alimaliza Game.
Jay-Z ambae ni mtu wa karibu sana wa Obama
kati ya wanamuziki wa Marekani, hivi karibuni alihost tamasha la kumchangia
Obama katika kampeni zake na akatokea kwenye tangazo la kusapoti kampeni za
Obama.
Jay- Z yuko mstari wa mbele katika
kuhakikisha kuwa Barack Obama anarudi White house na hata katika message ya
matumaini aliyoiachia Obama masaa kadhaa yaliyopita Jigga anaonekana kuifanyia
kazi na kuakisi kile alichosema Mr. president.
Obama amewapa nguvu wapiga kura kwa
kujiweka katika nafasi ya mpiga kura kisha akasema, “na mtaanza kuona nguvu ya
kura zetu. Wakati rais anaingia ofisini mwanzoni, kile alichokipresent kwa
taifa ilikuwa ni matumaini. Unajua, matumaini ya watu wote nchini ambao
wangetazama na kujiona katika mambo yanayowezekana…sasa watu wanatumia haki
yao, na mtaanza kuona nguvu ya kura zetu. . He made it mean something for the
first time for a lot of people."
No comments:
Post a Comment