Kundi la Rick Ross na kundi la 50 Cent wafanyiana fujo kubwa, ilisemekana walirushiana risasi .



Wakati jiji la Atlanta likishangweka na tukio kubwa sana la utoaji wa tuzo zinazojulikana kama BET Hip Hop Music Awards zilizotolewa weekend hii kwa kurekodiwa zikiendelea ili zirushwe kwenye TV October 9, nje ya ukumbi katika maeneo ya parking kulitokea fujo kubwa iliyowajumuisha wafuasi wa Rick Ross na wafuasi wa 50 Cent ambapo milio ya risasi ilisika.
Hali ya kutoelewana kati ya the big boss wa MMG na mtu mmoja backstage ya BET ndio inayosemekana kuwa ni chanzo cha vurugu hizo, ambazo baadae zilihamia nje katika maeneo ya parking ambapo hali ilikuwa tete na ikabainika kuwa ni ugonvi kati ya wafuasi wa 50 cent na wale wa Rossey.

 Gunplay ambae ni swaiba wa Rossey alionekana anajeraha na taarifa za awali toka kwa mashuhuda zikasema rapper huyo toka Miami alikamatwa na police na akafungwa pingu, lakini mtu wa karibu wa Gunplay alikanusha report hiyo, na akasisitiza kuwa Gunplay hakukamatwa na police.
Wakati hizo varangati zinaendelea huko nje, muda huo huo huko ndani shangwe ziliendelea kama kawaida ikiwa ni taping ya tukio zima la BET Hip Hop Awards na hakuna mtu aliyeshtukia kama nje kulikuwa na fujo kubwa kiasi hicho.  
Wakati huo Buster Rhymes, Missy Elliot walikuwa stejini kuonesha heshima na kumkumbuka Chris Lighty ambae ni mdau mkubwa wa Muziki, meneja wa zamani wa 50 Cent na pia mtu wa karibu wa Fat Joe.
Katika tukio hilo 50 Cent na Fat Joe waliweka tofauti zao pembeni na wakapanda jukwaa moja kwa ajili ya kutoa heshima kwa marehemu Chriss Lyghty.
Hata hivyo msemaji wa kitengo cha Police cha Atlanta aliuambia mtandao wa TMZ kwamba ni kweli muda mfupi baada ya saa moja na robo usiku jumamosi hiyo hiyo, yalitokea mapigano kwenye  parking ya maeneo ya Atlanta Civil Center ambapo BET Hip Hop awards ilikuwa inarekodiwa. Lakini alisema hakuna aliyekamatwa na hakuna serious injuries, na akamaliza kuwa report za kuwepo na kurushiana risasi linaonekana kuwa sio la kweli.

No comments:

Post a Comment