Wakati joto la uchaguzi wa urais wa
Marekani linazidi kupanda kila sekunde na kila celeb kutoa maoni yake kwa yule
anaemsupport kati ya Romney na Obama, No one hit maker Alicia Keys ameamua
kuiweka hadharani kura yake baada ya kupima na kuona kuwa inafaa kumsuport yule
ambae anaona atafaidika nae akiwa rais wa United States.
Alicia keys ameweka wazi kuwa anamsuport
Barack Obama na kwa hali hiyo ndiye atakae mpigia kura yake. Pamoja na sababu
nyingine alizozitoa lakini swala la kuwawezesha wanawake na kuwaheshimu
lilichukuwa asilimia nyingi sana, na kuongezea na connection kati ya Obama na
umuhimu wa wanawake.
Alicia Keys alifunguka kiivo baada ya
kumaliza tu kuongea katika women’s Vote Summit huko Philadelphia ambapo alipiga
story na mtandao wa SOHH kuhusu umuhimu wa wanawake kuhakikisha sauti zao
zinasikika katika uchaguzi wa uraisi wa Marekani mwezi ujao.
Pamoja na kuweka wazi kura yake bado Alicia
aliwaambia wanawake wampigie kura yule wanajisikia ni bora zaidi kati ya
wagombea hao wa Uraisi wa Marekani.
“Nadhani sisi kama wanawake tunaulazima wa
kuitumia vizuri sauti yetu kusimama kwa ajili ya mtu ambae atatupa heshima
tunayositahili kama wanawake katika nchi hii. Tumepiga hatua kubwa sana kwa
miaka mingi na hakuna sababu ya kurudi nyuma tena.” Alisema Alicia na kuongeza
kuwa “obviously I’m an Obama Supporter.”
Alipoulizwa sababu zinazomfanya ampe nafasi
hii Barack Obama, alisema “he has been raised by a strong super woman; he
married a super strong woman; he’s raising two credibly strong women; so he is
personally connected to what is important with women’s issues.”
The R&B queen alimaliza kwa kusema
anadhani hicho ni kitu kikubwa sana na hawawezi kukiacha kiende hivi hivi. Keys
alisisitiza “tunatakiwa kuwa really, really, really focused katika kuhakikisha
kila mwanamke anaenda kumpigia kura mtu ambae tunajua atakuja kuendeleza
kutu-encourage sisi na kupata kila kitu ambacho tunastahili. Chochote kinyume
na hapo kitakuwa sio sahihi.” Alimaliza Alicia Keys.
No comments:
Post a Comment