HIZI NI BAADHI YA PICHA ZA MPAMBANO WA WABUNGE SIMBA vs YANGA







Wachezaji wa Timu ya Simba (Bunge) wakicheza kwa furaha huku wakliwa wamemzunguka kocha Mpya wa Timu ya Soka ya Yanga Mbeligiji, Tom Saintfiet baada ya timu hiyo ya Simba Bunge kuwashinda kwa goli 3-2 watani zao wa jadi Yanga Bunge katika mchezo wa hisani uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa ni mchango wao katika Tamasha la Matumaini ambalo linakusanya fedha kwaajhili ya kujengea Mabweni ya Wasichana Vijijini.
 
Saintfiet aliwasili uwanjani hapo na kuketi benchi la Yanga (Bunge) huku mashabiki wakishangilia kuwa timu hiyo lazima ishinde lakini ndio waliambulia kichapo cha goli 3-2.

 Wachezaji wa Simba (Bunge) wakicheza kwaito baada ya kuwafunga 3-2 Yanga (Bunge).
 Soka likiendelea uwanjani
 Kocha Mkuu wa Yanga Saintfiet akishangaa namna Simba (Bunge) walivyokuwa wakitandaza soka.
Soka la Wachezaji wa Simba (Bunge) na Yanga (Bunge) lilikuwa zuri huku vituko kibao vikishuhudiwa uwanjani lakini Mchezaji nyota wa mchezo alikuwa ni Joshua Nassari wa Simba ambaye awali alikuwa akicheza ndani na kipa wa Simba Idi Azan alipoumia na kutoka alikaa goli na kuokoa mikwaju 3 ya Penati kiasi cha mashabiki kumuita Kaseja na kuipa timu yake ushindi wa goli 3-2.

No comments:

Post a Comment