Hizi ni baadh ya info kuhusiana na kuzama kwa Meli ya MV Skagit.







Inawezekana taarifa za ajali ya boti ya Seagul iliyotokea Jana (July 18) mchana Zanzibar ukawa umezisikia au kuzisoma sehemu mbalimbali lakini kauli hii ya Waziri wa mambo ya ndani imetoka kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku jana.
Waziri Emmanuel Nchimbi akiongea kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku july 18 2012  TBC1 alisema “vikosi vya uokoaji vinaongozwa na mkuu wa jeshi la polisi Inspekta Jenerali Said Mwema vinaendelea na uokoaji”
Kuhusu watu waliopoteza maisha au kuokolewa Waziri Nchimbi amesema “Katika abiria wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 250 waliokua wamebebwa na boti hiyo, wameokolewa 124 wakiwa hai na waliothibitishwa na jeshi la polisi kufariki dunia ni saba tu, juhudi kubwa za uokoaji zinaendelea”

Wakati watanzania wakiwa hawajapona majeraha ya kuwapoteza ndugu zao katika ajali ya Meli ya Spice Islander iliyotokea Septemba mwaka jana, Meli nyingine ijulikanayo kama Mv Seagull imezama majini ikiwa safarini ikitokea Dar es Salaam kuelekea Visiwani Zanzibar.
Meli hiyo ambayo kwa mujibu wa taarifa za mwanzo  ilikuwa na abiria wapatao 200 imezama na mpaka wakati huu  harakati za uokoaji zinaendelea na watu wakiendelea kuokolewa huku wengine wakielea juu ya maji kwa msaada wa maboya. Ingawa taarifa za vifo hazijatolewa bado ila ukweli kwamba vifo vipo.
Tukija kuiangalia historia ya hivi karibuni ya Meli hii iliyozama jana tunajionea mwenendo wake mbaya kwani imesharipotiwa matatizo mengi kadha wa kadha lakini ndo hii imeendelea mpaka kupelekea hili la leo.


Mapema mwezi wa tano (12/05/2012) GAZETI LA MWANANCHI liliripoti kuzima moto kwa  Meli hii ikitokea Pemba kuelekea Unguja katikati ya maji na kusababisha tafrani kubwa kutoka kwa wasafiri waliokuwamo ndani ya meli hiyo na iliwalazimu kubakia melini mpaka ukarabati ulipomalizika ndipo safari ikaendelea.
Vipi baada ya tukio/ matukio ya mwanzo, hatua gani zilichukuliwa katika kuhakikisha usalama wa wasafiri unaongezeka na kupunguza matukio kama haya???



 Tunawaombea wote waliokutwa na mkasa huu na Habari zaidi juu ya ajali hii tutaendelea kukujuza...




Hii ndio MV Skagit ikionekana kwa angani jinsi inavyozama.
Hii ndio boti iliyozama. 
Hapa ni bandarini Zanzibar miili pamoja na abiria waliosalimika wakiwa wameletwa.
Uokoaji ukiendelea July 18 2012 usiku.
Miili na waliookolewa ikiwa imewasili Bandarini Zanzibar.
Imeripotiwa kwamba kwa saa mbili boti kadhaa za uokoaji zilishindwa kuondoka Bandarini kutokana na mafuta kukosekana, hapa ni mafuta yakiwa yamewasili.
Boti ikiondoka baada ya kupata mafuta.
Miili ikiwa imewasili.
.
 
 




 

No comments:

Post a Comment