FACEBOOK KUFUNGWA RASMI JULY 15 by Mark Zurkerberg embu cheki hiyo habari

KUFUNGWA KWA FACEBOOK.
Najua kwamba taarifa hii inaweza kumshtua kila mtu ambaye amekuwa memba wa mtandao huu kwa kipindi kirefu ila kwa hapa hakuna budi kukubaliana na huyu mtu ambaye aliuleta mtandao huu kwenye internet na sisi kujoin.

Nilikuwa naipitia habari hii huku picha ya Mark Zurkerberg ikiwa pembeni akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari nje ya ofisi yake na kusema "Mtandao huu umekuwa ukinisumbua sana maishani mwangu kwa kuwa kuna wengi wamekuwa wakilalamika kila siku. Tuliweka kikao kizito na kuamua kwamba ni lazima tuufunge mtandao huu wa Facebook kwa sasa. Kilikuwa ni kikao kigumu na kizito na hata kuufikia uamuzi huo lilikuwa ni jambo zito, ila kwa sasa hatuna jinsi. Ni lazima tuuzime ifikapo tarehe 15/7/2012" Mark alisema na kuendelea.

Najua wengi wanaweza wasiwe na furaha, ila ningependa kuwaambia watu kwamba kwa sasa inawapasa kuchukua kila picha ambazo wanazo kwenye facebook kwa sababu baada ya tarehe hiyo hawataweza kuziona tena. Ni wakati sasa wa watu kuwasiliana, kukutana na kutengeneza urafiki wa kweli" Mark alisema mbele ya waandishi wa habari.

Najua kama haujawahi kuisikia habari hii utakuwa umeshtuka kama ambavyo mimi nimeshtuka. Kipindi cha nyuma nilikuwa nikipuuzia kwa sababu tarehe ambazo zilikuwa zikitangazwa kwa mtandao kufungwa wala haukufungwa. Nafikiri kwa sasa inaweza kuwa kweli na si porojo kama ambavyo ilivyokuwa mwanzo kwa sasabu ni Mark Zuckerberg mwenyewe ndiye ameongea hayo pamoja na msaidizi wake Bwana Avrat Humarthi.

Najua kwamba nimefahamiana na watu wengi katika mtandao huu na huku wengine wakijua kwamba kumbe kuna mtu duniani anaitwa Nyemo Chilongani ila kwa hiki ambacho kinataka kutokea, kuna uwezekano wa kutokuwasiliana tena. Kwa sasa unaweza kuchukua kila details ambayo unataka kuchukua kutoka kwa marafiki zako ili hata kama mtandao utafungwa basi angalau uwe na vitu vidogo kutoka kwa marafiki zako.
Hizi si habari za kutunga bali ni uhalisia a mambo. Nimeamua kukaa kwa tahadhari huku nikisikilizia tarehe hiyo, kama itakuwa kweli basi hatutokuwa na budi kukubaliana na uhalisia wenyewe ila kama ni uongo au wakighairi kuufunga, basi kuchati tutaendelea kama kawaida.

Nimeamua kuwataarifu kwa kuwa naamini ni asilimia kubwa ya watumiaji wa Internet Tanzania wanatumia simu zao na huwa ni vigumu kuingia katika mitandano mingine. Kwa wale ambao watasoma habari hii, naomba wawataarifu wengine pia.
Kwa sasa macho na masikio yangu yanaisubiri siku hiyo ili nione kama mtandao utazimwa kama ilivyotangazwa na Mark Zuckernerg au laa. Siku ikifika na ukafungua mtandao huu na kukuta haufunguki, usipate tabu kuutafuta, jua kwamba utakuwa tayari umezimwa.

Hatujui ni mtandao gani ambao utashika kasi katika kipindi ambacho Facebook hautokuwepo, hatujui ni mtu gani ambay atatufanya watu kuupenda mtandao wake, ila kwa sasa naona tumebakiza siku chache sana kuutumia tandao huu. Kwa haya yote ninasema Asanteni, kwa muelewa aelewe ila kwa asiyekuwa muelewa asielewe.
Mtandao utakapozimwa rasmi, kiukweli nitawamisi sana marafiki zangu na wale wote ambao waliwahi kuniwish siku yangu ya kuzaliwa.
Tukaeni kimya na kusubiri siku hiyo tuone kama utazimwa. Ikiwa haujazimwa, itakuwa poa sana ila ukizimwa, haina budi kujipanga upya.

ASANTENI.
 source: from mdau kupitia facebook

No comments:

Post a Comment