The West Coast rapper Game ambae alikuwa ni member wa zamani
wa G-Unit hakukawia kujibu Diss iliyotupiwa yeye na Young Buck kwenye ngoma
mpya ya boss wao wa zamani 50 Cent ‘My Life’.
Game amesema anajiona kama anaanza kufatilia kwa karibu ile
hard hitting yake “300 Bars” aliyotoa mwaka 2005 kwa ajili ya kudiss G-Unit.
Game ambae nae aliwahi kutoa ngoma inayoitwa ‘My Life’ akiwa
na Lil Wayne alipiga interview na Power 106 huko States na akaanza kwa kusema
yeye pia aliwahi kuwa na wimbo unaoitwa ‘My Life’, then bila kutafuna maneno
akafunguka zaidi.
“Labda ana kitu ambacho anataka kutuambia, unajua, kuhusu
maisha yake ya siri,” alifunguka Game baada ya kukiri kuusikia huo wimbo wa 50
Cent. “Hakuna mtu anaemuogopa 50. Tuwaulize watu. That’s really the best he can
do. You know what I’m saying? Buck yuko jela, hali yake ni hiyo, hawezi
kujitetea kutoka huko...Every now and again, unapata hii movie ya Zombie ambapo
haijalishi ni mara ngapi unawashot, wanaendelea kuamka...Freestyle yangu ya
mwisho ilikuwa kama ‘500 Bars’ na ilikuwa na kama na dakika 26. Freestyle
iliyoiua G-Unit, kila kitu, record lebel, nguo ni ‘300 Bars’ na natakiwa kwenda
na kuifanya mara mbili ya hapo niseme kiukweli kile nachotakiwa kusema. Kuna
mengi ya kusema.” That’s Game.
Kwenye ‘My Life’ ambayo ni ngoma mpya ya 50 Cent
akiwashirikisha Eminem na Adam Levine, mistari ya kwanza ambayo inawadiss Game
na Young Buck direct kwa kuwataja majina ni hii hapa.
"Yeah, 03, I went from back filthy to filthy rich /Man,
the emotions change so I can never trust a b*tch/I tried to help n*ggas get on,
they turned around and spit/Right in my face, so Game and/Buck, both can suck a
d*ck/Now when you hear 'em it may sound like it's some other sh*t/Cause I'm not
writing anymore, they not making hits".
Baada ya Game kutoka G-Unit mwaka 2003 hivi alianzisha
harakati nyingi za kuimaliza G-Unit na kutoa freestyle nyingi kama diss kwa
G-Unit lakini akazipa jina la ‘G-UNOT’ harakati zake ambazo watu wa mtaa
walitoa hadi t-shirt zenye maandishi hayo... ‘G-UNOT’.