Justin Bieber aonesha Tattoo mpya ya Bundi aliyochora mkononi, aiandikia maelezo.



Mwimbaji mwenye umri mdogo  toka Canada Justin Bieber ameongeza tattoo collection yake, tattoo ambayo ameichora kwenye mkono wake wa kushoto inaonesha picha ya bundi na kuiandikia maandishi yanayosomeka “Befo the paps get me.” Na alitweet maandishi haya.
Picha hiyo inaongeza idadi ya tattoo alizochora Bieber ikiwepo tattoo ya ndege mdogo kwenye hip yake ya kushoto, tattoo nyingine yenye picha ya Yesu, tattoo ya symbol ya kijapan inayoomaanisha muziki kwenye mkono wake wa kulia, na crown ndogo kwenye kifua chake upande wa kulia.
The Boyfriend hit maker anazidi kuongeza tattoo wakati anaendelea kusherehekea kuachiwa kwa album yake ya “Believe”.

Madonna azomewa Kwa kuwahamasisha mashabiki kumpigia Kura Obama, wengine wasusia tamasha lake.


mwimbaji mkongwe Madonna anazidi kuweka nguvu zake kumsapoti Barack Obama kwa kutumia japo dakika tatu katika tour yake ya MDNA kwa kuwa anaamini huwa anaongea na wapiga kura japo hayuko katika jukwaa la siasa. Weekend hii amekutana na changamoto baada ya kuzomewa na baadhi ya mashabiki waliokuwa katika show yake huko New Orleans alipowashawishi kumpigia kura Barack Obama.

Wakati watu wamenogewa na show, Madonna alistop kidogo na kuuliza, “nani ambae amejiandikisha kupiga kura?” Ikawa kama amepata ngazi ya kuendelea, “sijali nani mtakaempigia kura as long as mtampigia kura Obama.” Hapo baadhi ya mashabiki wakaanza kumzomea na wengine kuondoka na kuisusia concert yake.

Madonna alionekana kutokujali akaendelea, “seriously, sijali nani mtakaempigia kura…usiichukulie poa hii haki ya msingi. Nenda kapige kura.”

Inaonekana kabisa Madonna yuko serious na kumpigia kampeni Obama kila anapoona watu anaoamini ni wapiga kura kwa sababuu hii haikuwa mara ya kwanza kuwahamasisha watu waliohudhuria tamasha lake, labda nao wamechoshwa na maneno yake ya siasa.

Mwezi ulioopita alipokuwa Washington DC alitumia muda wake kuwazungumzia viongozi wa zamani kama Abraham Lincoln na Martin Luther King, Jr., akisema, “they killed him, as they do. … Ni ajabu kufikiria kuwa tuna rais ambae ni African-American ndani ya White House. Hao binadamu wema hawakufa for nothing.”

Ni kama muendelezo hivi kwa sababu majuzi kati Watu wengi ‘walimkritisaizi’ Madonna kwa kumuita Obama Muislam mweusi ndani ya White house alipokuwa katika tamasha lake kama kawaida. Lakini yeye mwenyewe alivunja ukimya na kuelezea, “nilikuwa Ironic nilipokuwa jukwaani. Kweli najua kabisa kuwa Obama sio muislam japo najua watu wengi hapa nchini wanaamini ni muislam. Na vipi kama angekuwa muislam? Point yangu ni kwamba mtu mzuri ni mzuri  tu haijalishi anaabudu nini. Sijali Obama ni dini gani- na wala mtu yeyote wa Marekani hatakiwi kujali kuhusu hili.

Presha ya kumrudisha raisi Barack Obama white house ama kumtupa kule na kumuweka Mitt Romney inazidi kupanda ikizingatiwa kuwa mwezi ujao ndio itafahamika, wanamuziki nao wanatumia kila gap wanalopata kusema kitu kumsapoti wanaemsapoti japo ndo hivo ukichanganya topic za burudani na siasa mara kwa mara ndio yanatokea haya yanamkuta Madonna.

Alicia Keys anunua jumba la kifahari la Eddie Murphy.


Lililokuwa jumba la Eddie Murphy ambalo sasa linamilikiwa na Alicia Keys

The R&B queen Alicia Keys anazidi kuthibitisha kuwa she is a girl on fire baada ya kulinunua jumba la kifahari la muigizaji maarufu duniani Eddie Murphy, jumba ambalo lilikuwa sokoni tangu mwaka 2004.
Kwa mujibu wa New York Daily News mwanadada huyo mkali wa kucheza na piano ndiye aliyenunua jumba hilo ambalo ni multi-million dollar Eglewood. Ripoti hiyo inaonesha kuwa mnunuzi ni Ms. Keys na haikumtaja Swizz Beat sehemu yoyote hivyo inaonesha kabisa kuwa Keys ameweza kwa nguvu zake mwenyewe bila kuwezeshwa.
Jumba hilo liko karibu na New Jersey, ambapo palikua maskani ya wakali kama P. Diddy na mwimbaji Wilson Pickett. Jumba hilo ambalo lilikuwa sokoni tangu mwaka 2004 lina vyumba vikubwa 32, vikiwemo vyumba nane vya kulala, sehemu za kuchezea racquetball na tennis, studio ya kurekodia muziki, elevator mbili, pool ya ndani, mabafu 10 full, na manne kama half-bath.
Eddie Murphy alitangaza kuuza jumba lake kwa mara ya kwanza mwaka 2004 kwa $30 million, na kuanza kushusha bei hiyo mara nyingi na mwaka 2010 akatangaza bei ya $ 12.75 million hiyo ni baada ya soko la nyumba za kifahari kushuka sana kuanzia mwaka 2008 kulipotokea anguko la kiuchumi marekani.
Ripoti za kuaminika zinasema jumba hilo lilitangazwa kuingia sokoni tena mwaka huu kwa mpunga kiasi cha $ 14.9 ambazo inawezekana kabisa kuwa ndizo pesa alizolipa Alicia Keys kumiliki mjengo huo wa maana.
Itakuwa kama Alicia anajiandaa kuwa na familia kubwa zaidi akiwa na mmewe Swizz Beats coz hiyo idadi ya vyumba vya kulala, ni crib ya maana sana hasa kifamilia. Hongera zake!

Chris Brown amuajiri Karrueche Tran kuwa designer wake wa nywele na nguo



Inaonekana kama hit make wa don’t wake me up Chris Brown hajakubali kabisa kuwa mbali na ex girlfriend wake Karrueche hata kama sio kimapenzi tena.
Kwa mujibu wa Hip Hollywood Chris alimpa ajira kuwa stylist wake, na Karruache Tran aliipokea ajira hiyo na kumdizainia mtindo wa nywele kwa ajili ya kufanya photo shoot inayoonekana ni the latest kwa Chris. Ajira hii inasemekana kuwa haina mahusiano na maisha yao ya kimapenzi bali ni kama wameamua kufanya biashara tu kwa kuwa Chris anahitaji designer na K.T ni mkali upande huo.
Watu wa karibu wa wawili hao wameendelea kukanusha kwa msisitizo kuwa hakuna kinachoendelea kati yao na kwamba Chris Breezy bado yuko na Rihanna wake na anavyokuwa karibu na K.T haimaanishi kuwa wanataka kurudisha mahusiano yao.
Kwa kawaida inaleta maswali kwa wengi hasa ukizingatia Chris alitamka hadharani tena kupitia video aliyoirekodi kuwa anampenda pia Karrueche japo inabidi tu amuache ili aende kwa Rihanna, na hivi karibuni walionekana anatoka kwake akiwa na K.T na kumsindikiza na ikasemekana mrembo huyo alienda kuchukua vitu vyake kwa Chris asepe kwa amani. Ila hii sasa ya kumpa ajira ya kuwa stylist wake katisha zaidi.

P’Square wajibu tuhuma za kumuua mama yao ili wapate umaarufu zaidi na pesa.



Imekuwa kawaida sana siku hizi kusikia watu wakizungumza kuhusu msanii flani ambae amefanikiwa sana, na stori huwa ni kwamba alienda kwa babu au ni freemason au kamtoa kafara ndugu yake ama hata wazazi wake ili apate umaarufu huo na pesa. Hali hiyo imewakumba wasanii mapacha waliofanikiwa sana kimuziki P’Square ambapo baadhi ya watu wamekuwa  wakisema wasanii hao walimtoa kafara mama yao ‘eti’ ili wazidi kuwa maarufu na wapate pesa zaidi.
P’Square ambao wanazidi kupata mafanikio kila dakika na kuuteka ulimwengu taratibu, walijibu kwa hasira tuhuma hizo, hivi ndivyo walivyoandika;
“Tunajisikia vibaya sana kujua kuwa mama yetu hayupo tena. Lakini sisi ni akina nani hadi tumuulize Mungu muweza wa yote. Kwa desturi, tulitakiwa tumzike na sio vinginevyo. Ila tu imetokea mapema sana. Kiukweli, kifo chake kilikuwa pigo kubwa kwetu.
“Then, ni mbaya sana kusikia kwamba watu wanatutuhumu sisi kwa kuwa chanzo cha kifo cha mama yetu. Hatumlaumu mtu yeyote. Watu wako huru kusema kile wanachotaka kusema. Tumeanza kushangaa endapo kuna kitu ambacho kingeweza kutusababisha tutumie maisha ya mama yetu.
Maisha yake hayawezi kupimwa kwa kiwango cha pesa wala umaarufu. Kwa hiyo jibu letu kwa swali hilo ni kwamba hatuna mkono wowote katika kifo cha mama yetu. Tunakilaumu kifo tu kwa kumnyakuwa mama yetu, na kama isingekuwa hivyo watu wasingetunyooshea vidole sisi. Alikufa baada ya kuugua ugojwa kwa muda mfupi sana.”
Haya ndiyo maelezo waliyoyatoa mapacha hawa kutoka Nigeria wanaotamba na ‘Beautiful Onyinye’ na ngoma kibao kiasi cha kunyakuwa tuzo kibao na kuongeza umaarufu na mpunga.
Tujiulize hivi mtu akipata umaarufu na mkwanja inakuwaje akipata tatizo basi inasemekana alitoa kafara, hata akifa yeye mwenyewe utasikia “ooh…freemason wamekasirika wamemchukua”. Duh, we need to think big though dunia ina mambo mengi na hayo yanaweza kuwa ni kati ya hayo mengi na huenda yanatokea kweli kwa baadhi ya watu.

President Obama Challenges Musicians To Get Political



 President Barack Obama during "Ask Obama Live"


President Obama is a big believer in the power of music to influence change — even if he doesn't exactly have the time to update his iPod.
When MTV News' Sway Calloway interviewed the president for "Ask Obama Live: An MTV Interview with the President" on Friday, he brought up the current state of politically conscious music. Bob Dylan, Public Enemy and Rage Against the Machine all made their mark in years past, but Sway wondered if Obama thought any current artists were effecting social change through their music.


"You know, it's an interesting question. We haven't seen as much directly political music," Obama admitted. "You know, I think the most vibrant musical art form right now over the last 10, 15 years has been hip-hop. Some folks have kind of dabbled in political statements, but a lot of it has been more cultural than political. You've got folks like Springsteen who are still putting out very strong political statements, but I'd like to see a more explicit discussion of the issues that are out there right now, because music's such a powerful mechanism."

So who was Barack Obama listening to as an undergraduate? The king of reggae himself, Bob Marley.
"I remember in college listening, and not agreeing with his whole philosophy necessarily, but raising my awareness of how people outside of our country were thinking about the struggle for jobs and dignity and freedom," Obama said of the iconic "One Love" singer.Obama referenced the '70s and the youth's sense of engagement in the anti-war movement that manifested in the era's protest music.
"I would hope that we're gonna see more of that," Obama said. "You can set the world on fire in a positive way."

Usher Buys $12k Puppy At Charity Gala, Donates Private Dance Lessons




 


Usher could not resist getting a new puppy Thursday night. The "Numb" singer purchased a female Goldendoodle for $12,000 at the Second Annual Pencils Of Promise Gala in Guastavino's in New York.

[Related: Usher & Shakira to replace Christina & Cee Lo on "The Voice" Season 4]
Usher boasted about his new pet on his Twitter page. "All in the name of [canine] fun! It took me 2 years but I outbid everyone this year to bring Poppy home to Ush," he wrote. The name Poppy is inspired by the event title, Pencils Of Promise (PoP).
According to People, Usher outbid former "Gossip Girl" actress Jessica Szohr. After Usher initially offered to buy the puppy for $10,000, Szohr raised the stakes to $11,000, prompting the R&B pop star to increase his bid to $12,000.

[Related: Usher, Jennifer Hudson highlight Whitney Houston tribute to air in November]
But Usher didn't just make a monetary donation to the organization, he is also volunteering his time. Two gala attendees each won private dance lessons with Usher for $65,000 each.
Usher's hefty charitable donation will help Pencils Of Promise's efforts to build 100 schools. So far, it has built more than 50.

New York nanny attempted suicide in front of dead children's mom: police



 General view of the apartment building where Yoselyn Ortega lives in New York, October 26, 2012. REUTERS/Eduardo Munoz
 General view of the apartment building where Yoselyn Ortega lives in New York.


The nanny suspected of slaying a Manhattan professional couple's two young children began stabbing herself as the mother entered the bathroom and began screaming when she saw the dead bodies in the bathtub, New York's police commissioner said on Friday.
The nanny, YoSelyn Ortega, had been employed by the family of Kevin and Marina Krim for two years before she killed their children and attempted suicide on Thursday in the family's luxury apartment, Police Commissioner Ray Kelly said.

Ortega, who lived with her son and sister near the Krims' apartment off Central Park, has been a naturalized U.S. citizen for a decade, Kelly said, adding that she had been referred to the Krims by another family.
New York police were hoping to interview the critically wounded nanny later on Friday, said an NYPD official who requested anonymity. Ortega, 50, has not been charged because police have not been able to interview her.
"We know now that the nanny began to stab herself as the woman entered the bathroom," Kelly said. "We initially thought it was, it had already been done, but now information is coming out that she did it as the mother entered the room."
Ortega remains the prime suspect in the stabbing death of the two children, Leo, 2, and Lulu, 6, Kelly said.
Marina Krim had entered the apartment at about 5:30 p.m. Thursday with her 3-year-old daughter, returning home after Ortega failed to meet her as planned at a local dance studio with the two other children.
Krim saw that the apartment was dark and returned to the lobby to ask the doorman if the nanny and kids had gone out, Kelly said. The doorman said no, and she returned to the apartment and went into the bathroom, he said.

Police spokesman Paul Browne said the children suffered "multiple stab wounds," and were pronounced dead after being rushed to a nearby hospital.
Kevin Krim, the children's father and an executive with CNBC, had been heading home from a business trip, He was met by police at the airport and notified of the killings, police said.
A spokesman for CNBC released a statement Friday expressing the "sadness we all feel" for Krim and his wife. The couple's "unimaginable loss ... is without measure."
Marina Krim, whose Facebook page lists her as originally being from Manhattan Beach, California, taught art classes to children, according to a website for the Hippo Playground Project, a New York organization where she volunteered.

She also maintained a photograph-laden blog to document her daily life with her children, with the final entry dated Thursday, three hours before the discovery.
"Leo speaks in the most adorable way possible," she wrote. "And he does things like, '(I) want a fresh bagel' and 'Lito (what he calls himself) wants cold milk' and most adorable of all, 'No thank you' - he never uses 'No' alone, it's always paired with 'thank you.'"
The blog was later blocked from public view.
A source at NBC News confirmed that the blog - which contains pictures of the Krim family - was Krim's.

Jumba la kifahari la Michael Jackson lauzwa mabillion kibao, ndipo alipofia Michael.



Kwa muda mrefu matajiri wengi walitamani kulinunua jumba la kifahari la marehemu Michael Jackson ambalo pia linakumbukumbu kubwa kwa kuwa ndipo alipofia mfalme huyo wa Pop, sasa jumba hilo limepata mnunuzi na limeshalipiwa mkwanja wote unaostahili.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ jumba hilo limenunuliwa na Steven Mayer ambae ni tajiri mkubwa na muwekezaji katika masuala ya bank.
Vyanzo mbalimbali vinaonesha kuwa jumba hilo limeuzwa kati ya dola za kimarekani million 17 na dola million 20, na lilikuwa limepangwa kuuzwa karibia dola za marekani million 24, ambazo zikibadilishwa kwa shilingi za kitanzania yatakuwa mabilioni kibao.
Inaonesha kuwa mnunuzi huyo anahamu kubwa ya kuingia katika jumba hilo kiasi kwamba amehamia wiki moja kabla ya umiliki wa mtu aliyekabidhiwa kuiangalia haujafungwa rasmi.
Kinachofurahisha zaidi ni kwamba muuzaji nae amemruhusu Mayer ahamie kwenye jumba hilo hata kabla hajasitishiwa rasmi umiliki ama uangalizi wa jumba hilo la kifahari, japokuwa anasitasita kwa kuwa anaona ni risk kwake.
Steven Mayer anaonekana analipenda sana jumba hilo kati ya matajiri wengi ambao walikuwa wanalitamani jumba hilo kwa hiyo kwa bei yoyote alikuwa tayari kulinunua na kushare baraka za Michael Jackson kwenye mjengo huo.

Lil Wayne alazwa hospitalini mara mbili ndani ya saa 24, wengine wasema sababu ni ‘drug overdose’.



Rapper mkali toka YMCMB Lil Wayne ameripotiwa kulazwa hospitalini mara mbili ndani ya saa 24 kwa kile ambacho kinaelezwa kuwa ni ‘seizure’, iliyompata kwa mara ya pili akiwa ndani ya private jet akitokea Texas kwenda LAX...
Mtandao wa TMZ uliambiwa na mtu wa karibu wa Weezy kuwa ndege hiyo ilikatiza safari yake na kuelekea Louisiana baada ya hali ya mkali huyo wa michano kubadilika ambapo alipelekwa hospitalini haraka kwa matibabu.
Hata hivyo taarifa za awali toka hospitalini hapo zilionesha kuwa Lil Wayne anaendelea vizuri na muda wowote angeweza kutolewa hospitalini hapo.
Tofauti na ugonjwa ambao watu walikuwa wanajua ndio unaomsumbua Weezy, Management yake ilitoa tamko kuhusu kile kinachomsibu rapper huyo baada ya taarifa za ku-seize hapo jana kwa mara ya kwanza.
“Lil Wayne aliweza kutolewa hospitalini baada ya matibabu kwa ajili ya maumivu makali ya kichwa na vilevile upungufu wa maji. Yuko nyumbani  amepumzika chini ya uangalizi wa daktari na atarudi kazini hivi karibuni. Ana-appreciate fans wake kwa sapoti yao na anawapenda.” Hilo ndilo tamko la management yake.
Ripoti zinazohusu hali ya Weezy kulazwa kwa mara ya pili hospitalini kwa ugonjwa wa ‘seizure’zilisambaa katika mitandao mbalimbali na watu wakatoa maoni tofauti tofauti kuhusu hili kwa sababu ugonjwa huu unaconnection kubwa sana na matumizi ya madawa ya kulevya.
Wengine waliuliza ‘could it have been a drug overdose??” lakini taarifa za kitaani tu zinasema alikuwa anakunywa sana siku hiyo na kuwa wanaunganisha ugonjwa huo na matumizi ya vilevi na madawa ya kulevya.
Mshindi huyo wa tuzo za Grammy aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo kama taarifa za management yake zilivyosema.
Matumizi ya madawa ya kulevya yamekuwa yakiwatesa sana mastaa nchini Marekani, hali hii ndiyo  inawafanya watu waunganishe hali ya afya ya Lil F.Baby na kutumia madawa ya kulevya kupita kiasi ‘drug over dose’.

Janet Jackson afuata nyayo za Michael Jackson, abadili dini kimyakimya na kuwa Muislam.


Janet Jackson baada ya kubadili dini kimya kimya

Mshindi wa tuzo za grammy mara tano Janet Jackson ambae pia ni mdogo wake Marehemu Michael Jackson, ni kama anafuata nyayo za kaka yake hata katika maswala ya imani.
Kwa mujibu wa muandishi mashuhuri wa Uturuki, Adam Oktar, Janet Jackson amebadili dini na kuwa muislam kimyakimya na ameamua kuwaficha fans wake katika hili.
Taarifa hii imekuja wakati Janet Jackson anasubiri kufunga ndoa na millionaire wa Qatar ambae ni mchumba wake wa sasa Wissam Al Mana. Na taarifa zinasema kuwa wawili hao wanatarajia kufunga ndoa huko Doha Qatar mapema mwaka kesho kwa kufuata imani na misingi ya Kiislam.
Chanzo kimoja kimesema wawili hao wanatarajia kutumia mkwanja kiasi cha dola za kimarekani million 3 kuzungukia kwa ndege wageni watakaohudhuria takribani 500, na kila mgeni atapewa zawadi ya kuonesha kumbukumbu ya ndoa hiyo na shukurani kwa kufika katika sherehe hiyo, zawadi hiyo inatarajiwa kuwa saa ya mkononi yenye thamani ya dola za kimarekani 10,000….ambazo ni kama fedha za kibongo zaidi ya million 15 kwa hiyo saa moja.
Kwa hali hiyo inaonesha kabisa kuwa wageni hao wataikumbuka sana ndoa hiyo ya mwanadada Janet Jackson na Millionaire wa Qatar Wissam Al Mana.

JUSTINE BIEBER ASHTAKIWA NA MTU ANAEDAI KUWA BABA WA GF WAKE, ETI ALIMUIBIA CREDIT CARD ILI AKUZE PEN*S YAKE”.


Justine Bieber

Katika hali ambayo inaonesha kuwa ni kituko cha mwaka, ama kichekesho flani tu ambacho obvious kinaonesha kutokuwa na ukweli, mtu mmoja ambae anadai kuwa ni baba mzazi wa girlfriend wa Justine Bieber mrembo Selena Gomez amefungua kesi mahakamani pande za Michgan.
Mtu huyo alifungua kesi yenye mambo mengi ya kushangaza, na pamoja na malalamiko yake pia yamewahusisha mastaa wengine wakubwa, haya ni kati ya malalamiko ya mtu huyo.
…“Bieber alinikopa $ 426.78 na hajawahi kunirudishia. Hizi pesa zilitumika kwa ajili ya kufanya abortion kwa sababu Justine Bieber alimpa binti yangu ujauzito kwenye chumba changu.”
…“Usher Raymond alikuja nyumbani kwangu tarehe 4, july 2012 na akaniingilia kinyume na maumbile na firework na akaiwasha in my anal area wakati huo anapiga makelele na wimbo wa Kate Perry Firework kwenye ngoma ya masikio yangu.”
…“Bieber aliiba credit card kwa ajili ya kununua cocaine kwa ajili yake na Sean P-ditty Combs.” Duh hapa alimaanisha P-Diddy, it’s funny heh!!!
….“Bieber pia alifanya pen*s enlargement kwa credit card yangu aina ya  ‘American express’.”
Lakini pia eti Bieber alimcheat binti yake na kutoka na Rihanna, Ke$ha na Penelope Cruz.
Hata hivyo mwisho wa malalamiko hayo akamaliza kuwa… “I’m an emotional mess…marekani inabidi isimamishe biashara ya muziki wa Bieber.”
Document ya kesi hii imenaswa na mtandao wa TMZ na hii ni document ambayo ni ya ajabu na ina malalamiko yasiyo ya kweli hata kwa kuyasikia tu, na inawezekana hayajawahi kutokea mahakamani hapo.
Kwa hiyo TMZ iliona hakukuwa na haja ya kumtafuta Bieber kumuuliza haya kwa sababu ni obvious uongo mtupu.

Niga C wa Jambo Squad aelezea sababu za kuachia wimbo wa ‘Dogo Mbumbumbu’, ndiye alimbatiza jina la Dogo Janja.


Niga C
Member wa kundi la Jambo squad lenye base yake Arusha City, Niga C amefunguka sababu zilizofanya aachie wimbo unaoitwa ‘dogo mbumbumbu’ambao ni diss direct kwa msanii aliyepata umaarufu akiwa na umri mdogo kwa jina la Dogo janja ambae sasa hivi anaitwa ‘Janjaro’ baada ya kudai umri hauruhusu tena kuitwa dogo.
Katika interview aliyofanya na Josefly mtangazaji wa radio Victoria Fm ya Musoma, Niga C alisema yeye ndiye aliyembatiza jina la Dogo janja na sasa aliamua kumbadilishia jina tena kwa sababu alibadikilika kitabia baada yakupata mafanikio.
“Unajua hata hili jina la dogo janja mimi ndiye niliyembatiza, nilimpa wimbo wangu unaoitwa sijisikii kufanya mapenzi na hapo ndipo jina la dogo janja lilipoanzia sasa dogo anajisikia kwamba akitoka akishapata mambo flaniflani, siunajua maskini akipata matako hulia mbwanta, ushansoma, dogo anazingua dharau nyingi nini na nini. Kwa mimi sio kwamba nimemponda pale nimemuelimisha tu. Mimi ndiye niliyempa jina la dogo janja nimemvua hilo jina nimempa dogo mbumbumbu, lakini haina maana kuwa namchukia kwa sababu nauhakika atakuja tu siku si nyingi si unajua yule ni mtoto tu. Kwa hiyo ile sio beef kwa sababu hata ukisikiliza mashairi nilioimba pale sio beef nimeongea ukweli, ningekuwa namchana mchano mwingine tofauti hapo ingeonekana ni beef. Lakini yule ni mdogo wangu nililalala nae kitanda kimoja, sahani moja tumekula, nimembeba mgongoni yule akiumwa mimi, kwa hiyo anapokuwa na kosa lazima niwe namwambia na lazima niwe namuadhibu na hapaswi mtu mwingine yeyote kuingilia kwenye swala hili, so sio beef na sio nimemdiss, nimemuelimisha kama mdogo wangu.”
Alipoulizwa kama alishawahi kuwasiliana na Janjaro baada ya kuachia hiyo ngoma ya ‘dogo mbumbumbu’ mkali huyo toka Jambo Squad wanaotamba na ngoma kibao ikiwemo Mamong’oo alifunguka, “siwezi kuwasiliana nae kwa sababu kilichosabisha nikaachia hiyo ngoma yake ni dharau zake yeye, kwa hiyo nimeshaanchia ngoma japo yeye alishanitumia message kibao yeye na meneja wake yule Ustadh Juma za matitisho matisho nini, lakini nauhakika kwa sababu yuko pale sasa hivi lakini akipata matatizo mi ndio mtu wa kwanza kunipigia simu na mimi ndio mtu ambae namsaidia siku zote yani, ushansoma, kwa hiyo mimi sioni hatari, sioni hatari yani.”
Niga C alifunguka mengi ikiwa ni pamoja sababu zilizopelekea Jambo squared kutokuwa na wa muziki na kwamba siku zote wao meneja wao ni Mungu.

Utata: Chris Brown aonekana akitoka kwake akiwa na Karrueche Tran na kupiga nae misele “K.T alienda kuchukua vitu vyake vilivyobaki asepe!!?”




‘Don’t work me up’ hit maker Chris Brown anazidi ku-make headlines kwa story ya mapenzi kati yake na ex girlfriend wake Karrueche Tran japo alitangaza kuwa amemuacha na kurudi kwa Rihanna. Juzi asubuhi Karrueche na Chris Brown wameonekana wakiwa pamoja tena wakitokea kweye mjengo wa Breezy na kuelekea katika gas station.

Wawili hao walitokea nyumbani kwa Chris Breezy wakiwa katika magari mawili tofauti na walionekana hawana wasiwasi na mtoko wao na wala hawakuogopa camera za paparazzi hadi waliposimama kwenye gas station, na inasemekana kuwa walipotoka hapo walielekea studio pande za Burbank, Calfornia.

Hii imeleta utata na kuonekana kama ni tamthilia ya ‘kifilipino’ ama ndo hivyo tena Chris anakula kotekote kwa Rihanna na kwa model Karrueche Tran kwa sababu alisema anawapenda wote, na wote wanampenda pia!
Rafiki wa karibu wa Chris aliiambia Hollywood Life, “Hell no, hawako pamoja(Chris na Karrueche). Yuko na Rihanna na wala hatoki na Karrueche kimyakimya. Karrueche alitaka favor na akafanya kwa ajili yake, pia akataka asindikizwe kwa Chris Brown ili achukukuwe vitu vyake vilivyobaki asepe. Ain’t no funny business between them.” Alisema huyo rafiki yake Chris B na kusisitiza, “he just helped her out one time with something and she needed to get her sh**t. No big deal.”
Lakini pia rafiki wa karibu wa Karrueche alipoulizwa alisema, “anachofanya Karrueche ni kuchukua vitu vyake kwa Chris and trying up some loose ends with Chris. Ni hivyo tu. Chris bado anasehemu kwenye maisha ya K.T ndiyo lakini she is strong kuendelea na kuyafanya hayo yawe yamepita, na najua anataka iwe hivyo.”
Tunaweza kujiuliza muda wote huu alikuwa hajafata vitu vyake kwa Chris, sasa si ilikuwa ni time ya Rihanna kutumia the same room aliyokuwa anaitumia Karrueche kwa Breezy? Hapo rafiki yake Karrueche akatoa majibu kiana, “Chris hakuwepo wikendi hii ili K.T achukue vitu vyake, kwa hiyo imebidi afanye leo. Inamuumiza kidogo kumuona Chris na nauhakika no matter what anyone says bado wote wanafeeling kwa kati yao.”
Pamoja na maumivu anayoyapata Karrueche rafiki yake anaamini kabisa kuwa yatapita tu soon na atamsahau, “but anyway, he’s a dog and hopefully this is her time around his a**.” Alisema best friend wa Karrueche Tran.

South Korea Hopes for 1st Rocket Launch Success Friday.

 

 The South Korean KSLV-1 rocket sits on the launch pad during ground tests before its first launch in 2009.


South Korea aims to join the ranks of spacefaring nations this Friday (Oct. 26) by blasting a small experimental satellite to orbit, according to media reports.
The country will attempt to loft a test satellite atop its Korea Space Launch Vehicle-1 rocket, or KSLV-1, from the Naro Space Center on Friday, weather permitting, South Korean officials said Monday (Oct. 22).
"We have confirmed after considerations of weather conditions and preparations for the launch that the launch will be possible on October 26," Minister of Education, Science and Technology Lee Ju-ho told reporters, according to South Korea's Yonhap news agency. "However, even through preparations will be made for October 26, the launch may be delayed if rainfall becomes imminent or very likely on the scheduled date."
The upcoming launch will be South Korea's third try to orbit a satellite with the KSLV-1, which was developed jointly with Russia and is also known as the Naro-1. Previous attempts in 2009 and and 2010 failed.
The spacecraft riding atop the rocket, called the Science and Technology Satellite-2C (STSAT-2C), weighs about 220 pounds (100 kilograms) and is designed to last up to a year in space. Its main purpose is to verify South Korea's ability to orbit a satellite and collect data in space, Yonhap reported.
If all goes according to plan, STSAT-2C will be delivered to an elliptical, 103-minute orbit that brings it as close to Earth as 186 miles (300 kilometers) and as far away as 932 miles (1,500 km), according to Yonhap.
Few of South Korea's neighbors are spacefaring nations; in Asia, only Russia, Japan, China and India have demonstrated the ability to put payloads into Earth orbit. Others have tried and failed, including South Korea's erratic rival North Korea, which made its third and latest attempt this past April.
Many analysts are suspicious of North Korea's attempted satellite launches — which have come in 1998, 2009 and 2012 — regarding them as thinly disguised tests of missile technology.

Obama : Romney is not to be trusted.


 
President Barack Obama

For weeks, President Barack Obama has criticized Republican nominee Mitt Romney for moderating his position on a range of issues throughout the campaign, but in a Tuesday afternoon rally here, he suggested that his challenger was not "trustworthy" enough to hold the nation's highest office.
"We joke about Gov. Romney being all over the map, but it speaks to something important. It speaks of trust. There's no more serious issue in a presidential campaign than trust. Trust matters," Obama said during his speech at a rally here. "You want to know that the person who is applying to be your president and commander in chief is trustworthy. That he means what he says. That he's not just making stuff up depending on whether it's convenient or not."
Obama added: "[Gov. Romney] is terrific at making presentations about stuff he thinks is wrong with America, but he sure can't give you an answer about what will make it right. And that's not leadership that you can trust."
 
The time and resources both campaigns are pouring into Ohio shows clearly that they consider the state a crucial component to reaching the 270 Electoral College votes needed to secure the presidency in November. While Romney has catered to the state by attacking Obama for federal regulations over the coal industry, Obama has hammered Romney for opposing the federal bailout of American auto companies on the brink of collapse four years ago.

About one in eight jobs in Ohio is tied to the auto industry, and the Obama campaign views the strategy as one that could help tip the state for the president. Both at the debate on Tuesday night and at the rally, Obama pointed to a 2008 op-ed Romney authored in the New York Times, "Let Detroit Go Bankrupt," that opposed offering federal funds to the struggling auto companies until they underwent a structure bailout, a move Obama contends could have forced those companies to go under completely.

Chris Brown amtukana fan aliyetaka autograph; ni baada ya kumpa mfano wa Rihanna, na kumuita ‘a wife beater’.



Kwa kawaida shabiki ndiye mtu anaefanya muimbaji yeyote awe staa kwa kumuongezea idadi ya mashabiki, lakini mambo hubadilika pale mmoja anapovuka mstari wa kuheshimiana.
Hii imemkuta shabiki mkubwa wa Chris Brown aliyekuwa na shauku ya kupata sahihi ya Muimbaji huyo kwenye CD cover yake lakini alijikuta anaambulia matusi baada ya yeye mwenyewe kuvuka mstari wa respect.
Shabiki huyo anaitwa Lucas Peter alisema kuwa walikuwa wanaangalia movie kwenye ukumbi wa Cinema wa Angeles’ Arclight  huko Hollywood na baada ya movie kuisha alimuona Chris Breezy anatoka ndipo alipoamua kumkimbilia ili asaini CD cover yake.
Shabiki huyo aliiambia Radar Online, “Bodyguard wa Chris B alinizuia na akanambia Chris asingeweza kusaini, mi nikamwambia mbona Rihanna huwa anasaini kila wakati. Hapo ndipo Chris aliposimama na akanipayukia ‘f***ot’.
Inaonekana mfano wa Rihanna kwake Chris ndio ulimkera zaidi, na hapo shabiki nae baada ya kutukanwa matusi akakasirika. Lucas aliendelea, “nilimuona Chris anaingia kwenye elevator na nikamuita ‘mpiga mwanamke’ na nikamuuliza kama atampiga Rihanna tena,” Lucas alifunguka bila kuyumbisha maneno, “Chris akasema, ‘I beat P***y’ halafu bodyguard wake akajaribu kunitishia kwa kusema, ‘na napiga wanaume pia.” Lucas alifunguka, baada ya hapo Chris akaendelea na safari yake.
Hapa unaweza kuona ni jinsi gani shabiki alionekana kukerwa na tusi alilopewa na Chris Breezy ambae inaonekana pia alikerwa na maneno ya kejeli ya shabiki huyo ambae hakupenda kukosa sahihi ya Chris. Inabidi kuwe na mutual respect kati ya shabiki na staa ili kuepuka haya.

Uliiona hii? ‘msanii wa bongo Movie asema anatamani Ney wa Mitego awe mumewe wa ndoa’.


Afsa

Ingawa Ney wa mitego ni jina ambalo wengi tunaamini kabisa halikubaliki kwa baadhi ya  wasanii wa bongo movie hasa wasichana baada ya kutoa wimbo wake ‘Nasema Nao’, na kufikia hatua ya kurushiwa maneno makali na baadhi ya waigizaji wa kike TZ, Afsa Omary Neema 20%  yeye sio tu kuwa anamzimia Ney wa mitego, lakini anataka awe mmewe wa ndoa kabisa and that’s that.
Kwa mujibu wa blog ya wajanja club katikati ya mwezi huu, Afsa Omary a.k.a Neema 20% kwa kinywa chake alifunguka, “Si siri nampenda sana Ney wa Mitego na natamani awe mume wangu wa ndoa hata kesho kama akikubali, kama ingekuwa wasichana tunaruhusiwa kuwatongoza wanaume na kuolewa nao basi mimi ningekuwa wa kwanza kwa Ney, ana mvuto na shababi.”
Sifa hazikuishia hapo, Afsa Omary a.k.a Neema 20 alidai kuwa anampenda mwanaume anaejiamini na mtanashati na muonekano anaouona kwa Ney wa Mitego na sio mtu mwingine na atafanya kila juhudi aweze kuishi na msanii huyo ambae kila akitoa wimbo lazima ulete gumzo.
Afsa Omary, Neema 20% kama wanavyomuita ni muigizaji aliyeibuka kupitia filamu ‘Furaha Iko wapi’ iliyotungwa na msanii wa bongo fleva Hamisi Kinzasa a.k.a 20 percent.
Habari ndiyo hiyo, ukweli anao mwanadada huyu mwenyewe kwa sababu hisia za mtu hazionekani tungepima tuhakikishe. 

The man bit the snake to death


An Indian Spectacled Cobra. 
 A Nepali man who was bitten by a cobra snake subsequently bit the snake to death, a local newspaper reported on Thursday (Aug. 23).

After being bitten by the snake, while he was working in his rice paddy on Tuesday, 55-year-old Mohamed Salmo Miya chased the snake, caught it and bit it until it died, the Annapurna Post reported, according to Reuters.

"I could have killed it with a stick but bit it with my teeth instead because I was angry," Miya was quoted as saying.
Miya, who lives in a village some 125 miles (200 kilometers) southeast of the Nepali capital of Kathmandu, was receiving treatment at a village health post at the time of the news report and was not in danger of dying from his snakebite. 

He will not be charged with killing the snake, a local police official said, because cobras (called "goman" in Nepal) are not listed as endangered in the country.

Clip of Twilight Breaking Dawn Part 2 "Inside Look" - Official Featurette [HD]

Clip of The Twilight Saga: Breaking Dawn - Part 2 TV Spot - Four Years (2012) - ...

Jay-Z na Beyonce wameshindwa kulifanyia biashara jina la mtoto wao “Blue Ivy”, mahakama yampa mtu mwingine ruhusa ya kulitumia.



Akili ya biashara iliyondani ya familia ya mastaa hawa the Diva Beyonce na rais wa Rock Nation Jigga ndiyo inayowafanya kuwa couple inayoingiza mkwanja mrefu sana kwa sababu hawategemei tu muziki bali kila kukicha wanawaza kuongeza vitega uchumi, lakini sasa wameshindwa kulifanyia biashara jina la mtoto wao Blue Ivy.

Couple hii inayomulikwa zaidi na camera za paparazzi na media kiujumla ilipanga kulisajili jina la mtoto wao Blue Ivy liwe alama ya biashara yao ‘trade mark’ muda mfupi baada ya mtoto wao wa kike kuzaliwa January 2012.
Ripoti zinasema Jay-Z na Beyonce walikuwa na mpango wa kuanzisha clothing line ya nguo za watoto na ingepewa jina la Blue Ivy. Lakini jina hili (Blue Ivy) linatumiwa kama trade mark na kampuni nyingine ililoko Boston inaloitwa Blue Ivy Events Company.
Boston’s Fox 25 imeripoti kuwa Jay-Z na mkewe Beyonce wameshindwa kabisa kulitumia jina hilo na kampuni ya Blue Ivy Events ndiyo iliyopewa leseni ya kuendelea kulitumia jina hili.
October 16, judge alimuunga mkono mmiliki wa Blue Ivy Events, Veronica Alexandra aliyekuwa analitetea mahakamani jina hili kama trademark ya kampuni yake.
Kwa hali hiyo Veronica Alexandra anayoruhusa kisheria kufanya biashara bila kuingiliwa na mtu yeyote kwa kutumia jina Blue Ivy Events Company, hivyo Jay-Z na Beyonce wamezuiwa kisheria kutumia jina hili katika kutangaza clothing line yao kwa ajili ya nguo za watoto.

Amber Rose ataja jinsia ya mtoto wao mtarajiwa ‘bila kukusudia’! Alidai ndoa kabla ya kujifungua.



Amber Rose ambae ni girlfriend wa Rapper Wiz Khalifa ameandika tweet kwa followers wake million 1.4 iliyotaja jinsia ya mtoto wao wanaemtarajia.  lakini katika tweet hiyo anaonesha kama hakuwa na plan ya kutaja jinsia ya mtoto huyo ila ni kama ameitaja accidentally,wanatarajia mtoto wa kiume.
Lakini hii inawezekana aliamua tu kwa sababu ameandika katika tweet moja hiyo hiyo message inayotaja jinsia ya mtoto wao mtarajiwa na hapo hapo anashtuka kama kataja bila kujua.
Tweet yake ya jumapili ilikuwa inasomeka “My friend Maria bought our Lil Boy this Slash onesie….Oops did I say Lil Boy???
Hata hivyo Media za U.S.A zimefatilia sana kujua jinsia ya mtoto mtarajiwa wa mastaa hawa, na wiki iliyopita gossip sites zilitangaza jinsia ya mtoto wao na kusisitiza kuwa wamefatilia na wamepata uhakika kuwa ni mtoto wa kiume na hii ni kutokana na shopping wanazofanya mastaa hawa ambapo vitu vinavyonunuliwa kwa ajili ya maandalizi ya mtoto wao inaonesha wazi kuwa ni mtoto wa kiume, hasa vitu vya rangi ya blue.

Lakini hata ukifatilia statement za Wiz Khalifa mwenyewe huwa anataja kiwakilishi ‘HE’ akiwa anamzungumzia mtoto wao japo hajawahi kusema kuwa ni mtoto wa kiume lakini hii pia ilikuwa inamaana. Mwezi August alimwambia rapper Colloway “You’re going to teach him how to rap.”

Hivi karibuni pia Amber Rose alipokuwa anazungumzia mipango yao ya kumpokea mtoto wao katika maisha yao alisema wanapanga kuoana kwanza kabla hajajifungua mtoto.
“Nah, hakuna tarehe iliyopangwa bado. Lakini tunaweza kupata license na kufunga ndoa kabla mtoto hajazaliwa, na tutafanya sherehe baadae kwa sababu italeta maana kwa mtoto kuzaliwa katika wedding na zaidi ya kuwa katika hii hali ya ujauzito tu. Watu wengine wanaharakisha na kufanya. Lakini njia zote zinawezekana” alisema Amber Rose ambae ni Ex girlfriend wa Kanye aliyezama kwenye bahari ya penzi la rapper Wiz Khalifa.

Hatimaye Justine Timberlake na Jessica Biel wafunga ndoa.


Wanandoa Timberlake & Jessica Biel

Safari ya mapenzi kati ya mkali wa R&B Justine Timberlake na muigizaji nyota Jessica Biel waliyoianza mwaka 2007 sasa imefika pazuri baada ya wawili hao kufunga ndoa na kuhalalisha mahusiano yao kama mke na mme.
Ndoa hiyo imefugwa Borgo Egnazia Resort nchini Italy katika jiji la Fasano. Mastaa hao waliwekeana ahadi za kuishi pamoja katika kila hali na kushuhudiwa na familia zao pamoja na marafiki.
Wanandoa hao wapya walionekana kuifurahia sana siku hii ya ndoa yao na kwa pamoja walisikika wakiwaambiwa watu “It’s great to be Married.”
Timbaland producer na mwanamuziki ambae ni swaiba wa Timberlake na mtu wanaeshirikiana katika muziki ni moja kati ya marafiki wa karibu waliokuwepo ukumbini.
Hakuna siku nzuri kama hii hasa kufunga ndoa na mtu ambae ulimpenda kwa siku nyingi na kuwa na ndoto ya kufunga nae ndoa siku moja na sasa ndoto hiyo imekuwa kweli, na hii ndiyo sababu ilimfanya Timbalake na mkewe Jessica kusema kwa pamoja “It’s great to be married.”

Rick Ross & Gucci Mane wamchana Young Jeezy ,wamtaka awape heshima.


Nitaurudia msemo uliozoeleka kuwa ‘adui wa adui yako ni rafiki yako kwa muda huo’ na hiki ndicho kinaonekana, kati ya vitu vinavyowaweka pamoja Gucci Man na Rosay sasa hivi ni ‘kila mmoja anabeef na Young Jeezy’.

Siku chache baada ya Gucci Mane kutoa wimbo aliupa jina la ‘Truth’ ikiwa ni diss moja kwa moja kwa Young Jeezy, sasa Rick Ross ameamua kumuongezea nguvu na kwa pamoja wametoa ngoma ya kumdiss Young Jeezy wakitaka awape heshima yao na ngoma hiyo wameibatiza jina “Respect”.
Katika track hiyo kuna mashairi ya moja kwa moja kwenda kwa Young Jeezy, ambapo Gucci alichana “Aint no way in hell I’ma let you desrepect me… Mad I’m fu**ng ur wifey” na Rick Rosay kiongozi wa May Back Music Group akaingia na verse yenye baadhi ya mistari kama “I push a button and them killers comin’/ Disrespect me, ni**as get nothing’.
Rosay na Young Jeezy wanabeef ambalo lilionekana waziwazi wakati wa kurekodi matukio ya BET Hip-Hop awards 2012 ambapo walifikia hatua ya kusukumana wakiwa back stage.
Mwenyewe Young Jeezy alizungumzia beef kati yake na Gucci Man mwanzoni kabisa mwa mwezi huu na akasema “ Najisikia kama kila mtu anamjua yule kijana, hakuna anaemchukulia seriously. Ana Ice Cream Cone usoni. Wanasema narudi nyuma. Mimi naenda mbele. And it’s crazy kwa sababu watakuita kwenye wimbo wao. Na usipotokea kwenye huo wimbo wao, hicho ndicho kinachotokea.”

Mastaa wampongeza Drake kwa kuhitimu High School.


Drake

Kweli elimu haina ustaa na inaweza kuwa kweli kabisa tena 99.9% kuwa ni ufunguo wa maisha, pamoja na kuwa na jina kubwa sana katika ulimwengu wa muziki na kuingiza mkwanja mrefu sana, bado Drake hakukubali kupitwa na elimu, na kwa kukomaa na vyote hivi karibuni amehitimu high school na kuongeza CV ya taaluma.
Kikubwa zaidi ni kwamba Drake ameweka hadharani alama alizopata, ambapo amesema amepata 97% kwenye mtihani wa mwisho na 88% kwenye course. hizi ni alama nzuri, kweli Drake sio kilaza.
Baada Rapper huyo kutangaza hadharani kuwa amehitimu masomo ya high school watu mbali mbali wakiwemo mastaa wa Hip Hop na mastaa wa Hollywood wamempongeza, na wakati huo huo wapo watu wengi ambao wameshangaa kwa sababu hawakujua kama anasoma.
hongera zako Drake, na huu utakuwa mfano mzuri wa kuigwa na baadhi ya wasanii hasa wa bongo, wanaoacha shule eti kwa sababu ya muziki.

Hiki ndicho Bonta angependa kitokee kwa makundi ya Hip Hop Tanzania, kuhusu alichosema Nikki Mbishi “No Comment”.


Bonta

Bonta a.k.a Maarifa hivi karibuni ameachia wimbo wake unaoenda kwa jina la ‘Tukutane Maktaba’ ambao umesababisha maoni mbali mbali kutoka kwa watu hasa kupitia mitandao ya kijamii kama facebook, wengi wakimpa big up kwa kazi yake, lakini pia alipata criticism toka kwa Nikki Mbishi wa Tamaduni Music ambae amekuwa akiandika status kuwamcriticise Bonta na baadhi Weusi.
Mweusi toka katika kundi la River Camp Soldiers alifanya interview na Josefly mtangazaji wa victoria fm iliyoko Musoma, kupitia kipindi cha Over drive.
The river camp doctor alifunguka mengi kuhusu ‘tukutane Maktaba’, kisha mtangazaji huyo aliuliza “baada ya kuachia ngoma yako watu wengi walionekana kuipokea vizuri kupitia mitandao mbali mbali ya kijamii na blogs mbalimbali, lakini kuna criticism, unamfahamu jamaa mmoja anaitwa Nikki Mbishi?” Bonta alijibu “ah, hiyo no comment, hilo siwezi  kuzungumzia kwa sababu kila mtu ana uhuru wa kuongea kitu chochote anachotaka kwenye nchi yetu, kwa hiyo no comment kwa hilo mtu wangu.”
Na kuhusu kile anachotamani kitokee kati ya makundi yote ya hip hop Tanzania ambacho kingemfanya aone kakundi yamepiga hatua Tanzania, alifunguka, “mi natamani kila kundi lifanye muziki wake na kila kundi litumie miguu yake kutembea kufika pale linapotamani na lisitumie mgongo wa kundi lingine, lisitumie midomo yao vibaya wala lisitumie freedom of speech vibaya, kila mtu afanye kazi yake na kila aheshimu kazi ya mtu, au sio, usitumie effort ya mtu ambayo ameshatengeneza ili upate negative publicity, at the  end of the day unajua mashabiki wako ndio mashabiki wangu, mashabiki wangu wataendelea kuwa mashabiki wangu na mashabiki wako wachache watakuja kwangu.”

Mikasa yamuandama Justine Bieber,Baada ya kuibiwa laptop kwenye show, sasa adondoka kwenye ngazi wakati anaperform.


Mikasa yamuandama Justine Bieber,Baada ya kuibiwa laptop kwenye show, sasa adondoka kwenye ngazi wakati anaperform.

Mikasa inazidi kuiandama tour ya ‘Believe’ ya Justine Bieber ikiwa ni siku chache baada ya kuibiwa laptop yake akiwa stejini huko Arizona Washington, sasa amepata mkasa mwingine baada ya kuanguka alipokuwa anaperform huko Saskatchewan Canada usiku wa October 17.

Bieber alikuwa anakaribia mwishoni kabisa kumalizia wimbo wake wa Beautiful aliokuwa anaupiga na Carly Rae Jepsen, msichana huyo alishuka kwenye ngazi za steji akiwa na Justine Bieber, lakini kwa bahati mbaya Bieber alimiss step moja kwenye ngazi akakosa balance na akaanguka.
Baada ya tukio hilo immediately Jepsen alimshika mkono Bieber na kumuinua, na mkali huyo aliweza kusimama na kuendelea kumalizia perfomance yake kama vile hakuna kitu kam hicho kilichotokea pale.
Mkali huyo ambae ni boyfriend wa Selena Gomez anatarajia kuendelea na tour yake ‘Believe’ hadi mwakani. na ratiba yake inaonesha kuwa baada ya hiyo show ya Saskatchewan ataelekea Winnepeg na Minneapolis kati ya October 18-20. na baada ya hapo anatarahji kuingia Ulaya around February 2013.