Expendable two iliyowashirikisha action movie stars kibao
wakiongozwa na Sylvester Stalonne (Rambo), Jean Claude Vanndamme, Jet-Li,
Arnold ShwazNiger, na wengine, imekumbana na tatizo la kisheria.
Waandaaji na
wawezeshaji wengine wanakabiliwa na mashtaka yanayotokana na scene ambayo
haikwenda sawa na kupelekea mtu mmoja kupoteza maisha na mwingine kujeruhiwa
vibaya.
Mtu mmoja anaejulikana kwa jina la Nuo Sun alijeruhiwa
vibaya katika mlipuko ambao ulisababisha kifo cha muigizaji Kun Liu, ambapo kwa
mara ya kwanza familia ya marehemu iliiburuza mahakamani ‘Expendable 2’ wakidai
fidia mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha kiasi cha dola za marekani 25,000.
Taarifa za hivi karibuni zinasema Nuo Sun ambae alijeruhiwa
vibaya na kupelekwa jijini Munich huko Ujerumani kwa matibabu akiwa chini ya
the best specialist amewafungulia mashtaka waandaaji na washiriki wengine wa
movie hiyo.
Katika mashitaka hayo yenye kurasa 12 Sun amedai kuwa,
“mlipuko na similar extra-hazardous activities vilisababisha tukio la hatari
juu ya rubber boat wakati wa kushoot sehemu ya pili ya filamu hiyo October 27,
2011.
“Kwa uzembe wa moja kwa moja wa washitakiwa, kutojali, na
matendo kinyume na sheria, mlalamikaji aliumia na kupata majeraha katika afya
yake, uwezo wa kufanya kazi, mshituko wa kiasi kikubwa na majeraha katika mfumo
wake wa fahamu, shingo, kichwa, mwili, mikono na miguu, majeraha yote haya
yanaweza kuwa ya kudumu, na majeraha haya yamesababisha na yanaendelea
kusababisha madhara katika fahamu zake na mwili wake kwa ujumla. Hivyo mlalamikaji
anadai fidia .” Haya ni baadhi ya maandishi yanayopatikana kwenye faili la
mashtaka lenye kurasa 12.
Akiwakilishwa na Robert M. Klein, Sun anadai fidia ya hasara
ya kipato chake kwa wakati uliopita, uliopo na ujao. Lakini pia anadai fidia ya
jumla zaidi ya $25,000, gharama za matibabu ya wakati uliopita, uliopo na hata
baadae, gharama za kuendesha kesi na mengine ambayo mahakama itaamua.
Baada ya mlipuko huo ulioua mmoja kati ya actors wa movie
hiyo na kumjeruhi vibaya Sun, uongozi na watayarishaji wa movie hiyo walitoa
tamko kuomba radhi na kuwaitakia pole familia ya marehemu na vilevile kuendelea
kusapoti kwa karibu sana familia na kumhudumia Sun akiwa hospitalini.
Hata hivyo Sun alikanusha kauli iliyotolewa na waandaaji hao
kuwa Jet-Li alikuwa pia karibu na mlipuko huo, na kusema hakuna star yoyote
aliyekuwa karibu na mlipuko huo.
No comments:
Post a Comment