Baaada ya mafanikio ambayo bado anaendelea kuyapata siku
hadi siku, Rihanna aamua kuichangia kiasi cha dola 1.75 milioni hospitali ya
huko kwao Barbados.
E! News imeripoti kuwa R&B Diva Rihanna ametoka kiasi
hicho kama kumbukumbu ya marehemu bibi yake Clara “Dolly” Braithwaite ambaye
alifariki kutokana na kansa mwezi June mwaka huu.
Mchango huo umeelekezwa kwenye idara ya ‘rediotherapy’
katika hospitali ya Queen Elizabeth iliyoko Bridgetown huko Barbados na hiyo
idara inatakiwa iitwe ‘Clara Braithwaite Centre for Oncology and Nuclear
Medicine’.
“Hii ni njia yangu ya kuirudishia Barbados .kwa namna ya
‘philanthropy’ kwa kusaidia muendelezo wa mpango huu wa kisasa, na naamini hii
itakuwa na faida kubwa sana kwa watu wa Barbados, itaokoa maisha na kuwafanya
waishi muda mrefu zaidi” , mesema Rihanna.
No comments:
Post a Comment