R&B diva Alicia Keys amekumbwa na msala wa kesi
inayohusiana na kuvunja sheria ya haki miliki, yaani copyright infringement kwa
kunakili bila ruhusa ya mmiliki baadhi ya mistari inayosikika kwenye wimbo wake
akiwa na Nicki Minaj ‘Girl on Fire’.
Keys anashtakiwa na mwandishi wa nyimbo anaeitwa Earl Shuman
ambae anadai kuwa Alicia Keys aliiba mistari miwili kwenye wimbo unaoitwa
“Lonely Boy” ambao aliandika akishirikiana na mwanamuziki Leon Carr na kurediwa
na Eddie Holman kwa jina la “Hey There Lonely Girl” mwaka 1970 na ikashika
nafasi ya pili kwenye Billboard chats enzi hizo.
Kwa mujibu wa blog ya blogger maarufu Friedman, Alicia Keys
alitumia sekunde mbili tu za kwenye wimbo halisi aliokopi lakini ndizo
zilizomsaidia kurekodi wimbo wake mzima wa ‘Girl on Fire.’
Mwandishi huyo mkongwe katika sanaa ya uandishi wa nyimbo
ambao kwa wenzetu walioendelea wanauheshimu sana ametoa ripoti kupitia blog ya
Friedman (show bizz 411) kuwa ameshafungua kesi mahakani akimshtaki Alicia
Keys, kampuni ya Sony Music waandishi Salaam Remi na Billy Kravan. Katika
mashtaka hayo Shuman ameeleza kuwa mshitakiwa(Alicia Keys) amevunja sheria kwa
kuingilia haki miliki yake kwa hiyo anahitaji fidia ya kazi yake, ikiwa ni
pamoja na faida iliyopatikana kwenye wimbo huo “Girl on Fire.”
Wakati mrembo huyo anahitajika kujibu mashtaka kwa pilato wa
huko Obama land, yeye anaendeleza mashambulizi ya kuumaliza mwaka na vitu
vikali na ameachia video yake mpya ya wimbo unaoitwa “Brand New Me” ambayo iko
kwenye album yake ya “Girl on Fire”.
No comments:
Post a Comment