Mwanamuziki toka Korea anayetamba na track yake ya Gangnam
style ambayo pia ndiyo video ambayo iliangaliwa na watu wengi zaidi kwenye
youtube mwaka huu, ameomba radhi kwa rap yake aliyofanya ikiwa inawatukana
wamerekani mwaka 2004.
Wakati anaendelea kupata heshima kubwa sana katika ulimwengu
kwa ngoma yake, media za Marekani ziliiachia hewani rap yake hiyo aliyoifanya
mwaka 2004, na muda mfupi baada ya habari hiyo kuzidi kumake headline PSY
alijitokeza na kuomba radhi mapema kwa wote ambao aliwakosea kupitia rap hiyo.
Alisisitiza, “I will forever be sorry for rapping the provocative anti-American
lyrics at his concert eight years ago.”
Aliendelea kufunguka, “kama navyojivunia kuwa Mkorea ambae
nilisomea Marekani na niliishi huko katika sehemu muhimu ya maisha yangu,
naelewa kujitoa kwa watumishi wa Marekani na wanawake kumefanya kulinda uhuru
na democrasia katika taifa na duniani.”
Varangati hili liliibuka baada ya media za marekani
kurudisha nyuma kumbukumbu za watu hadi mwaka 2004 ambapo Marekani ilipigana
vita na Iraq, na wakati huo PSY alikuwa bado hajafanikiwa sana kimuziki lakini
alipopanda jukwaani alirap, “Kill those f***ing Yankees who have been torturing
Iraqi captives, Kill those f***ing Younkees who ordered them to torture/Kill
their daughters, mothers, daughters-in-law and fathers/Kill them all slowly and
painfully.”
PSY alijitetea akasema kuwa aliandika mashairi hayo akiwa
katika mtafuruku mkubwa wakati wasichana wawili wa shule wa Korea na ilikuwa ni
wakati ule.
“Wimbo huo niliimba miaka nane iliyopita ulikuwa ni sehemu
ya hisia zangu kali kwa vita ya Iraq na mauaji ya wasichana wawili wa shule
raia wa Korea na ilikuwa ni ujumuisho wa upingaji vita kwa wakati ule.”
Hata hivyo mzee wa Gangnam Style anatarajia kupiga show kubwa
huko Washington katika tamasha la Christmas litakalofanyika December 21 na
kuhudhuriwa na rais Barack Obama na familia yake.
Muwakilishi wa White House amethibitisha kuwa Obama na
familia yake watahudhuria na wanatarajia kumuona PSY wa Gangnam Style akifanya
vitu vyake jukwaani.
No comments:
Post a Comment