Watangazaji wa kituo cha radio cha Sunrise cha jijini
Arusha wamegoma kufanya kazi kutokana na uongozi wa kituo hicho kushindwa
kuwatimizia matakwa yao ikiwa pamoja na kulipwa ujira mdogo na wengine kufanya
kazi bila kupewa mikataba.
Hii ni barua waliyoiandika:
Ndugu wanahabari sisi baadhi ya wafanyakazi wa Sunrise Radio
Arusha kuanzia tarehe 22/8/2012 tumeamua kugoma kuendelea kufanya kazi na Aspire
Media Company Limited ambao ndio wamiliki wa Sunrise Radio 94.8 FM Arusha baada
ya kushindwa kutimiziwa mambo kadha wa kadha tuliyokuwa tunayahitaji.
Mgomo huu ulianza kama mgomo baridi mnamo tarehe
10/8/2012 baada ya sherehe za wakulima nane nane na hii ni baada ya kutokea
tofauti kati ya mkurugenzi wa ufundi wa Sunrise Radio ndugu Dionis Idowa Sikutegemea
Moyo na kamati ya sherehe za wakulima nane nane mwaka 2012 ambao ndiyo
waliokuwa na jukumu ya kurusha matangazo ya moja kwa moja yaani live kutoka
katika viwanja vya taso nane nane Njiro.
Ndugu wanahabari mgomo huu umesababishwa pia na
kutofanyiwa kazi kwa madai ya wafanyakazi, wafanyakazi tumekua tukifanya kazi
katika mazingira magumu kwani:-
a) Tunalipwa mishahara midogo isiyokidhi mahitaji
(mshahara wa 100,000 na wengine 170,000)
b) Kufanyishwa kazi bila kuwa na mikataba, tukidai
mikataba tunapigwa tarehe
c) Kutokatwa makato kwenye mishahara kwaajili ya
pensheni
d) Baadhi ya wafanyakazi kufanyishwa kazi bila kulipwa
e) Hakuna overtime payment
f) Wafanyakazi kutishiwa kufukuzwa mara kwa mara pale
wanapodai haki zao
g) Hakuna likizo
h) Waandishi wa habari walioripoti live ya uchaguzi wa Arumeru
Mashariki tarehe 1/4/2012 kutolipwa posho zao hadi leo na wengine walidai na
hatimaye wakafukuzwa kazi
i) Mishahara wa wafanyakazi kucheleweshwa kulipwa kwani
utakuta mshahara wa mwezi huu tunaweza kulipwa mwezi ujao katikati au mwishoni
j) Mkurugenzi wa ufundi kutishia kumfukuza kazi mhasibu
kwa maslahi yake binafsi
k) Wafanyakazi wanaofanya vipindi vya usiku kutopewa
usafiri wakati wa kwenda na kurudi kitu ambacho kinamlazimisha mtangazaji
kulala studio kwa lazima
l) Gari la ofisi kutotumika kwa mahitaji ya ofisi bali
kwa maslahi ya mkurugenzi wa ufundi
m) Mishahara ya mwezi July ya baadhi ya wafanyakazi
kuzuiliwa kuanzia tarehe 1/8/2012 hadi leo hii tarehe 22/8/2012 kwa sababu
zisizo za msingi
Ndugu wanahabari, kwa madai hayo hapo juu sisi
wafanyakazi wa sunrise radio hatupo tayari kurudi kazini mpaka pale mkurugenzi
wa ufundi ndugu Dionis Idowa Sikutegemea Moyo atakapojiuzulu nafasi yake na
madai ya wafanyakazi yatakapokua yametatuliwa.
Dionis Idowa |
Tunaipenda sana Sunrise Radio bila kuwasahau
wasikilizaji wetu pia tunawapenda sana ila tumeona ni vyema kuyaweka bayana
haya yote ili mtuelewe na pia ni majibu ya baadhi ya maswali mliyokuwa
mnatuuliza wasikilizaji wetu wapendwa.
NDUGU WANAHABARI WAFANYAKAZI WA SUNRISE RADIO WALIOGOMA
KUFANYA KAZI IDADI YAO NI KUMI NA WAWILI (12) WAKIWEMO
a) WATANGAZAJI 4
b) MARIPOTA 2
c) WATU WA MASOKO 3
d) WAZALISHAJI WA VIPINDI 2 NA
e) MHASIBU 1
WAFANYAKAZI HAO WAMEGOMA KUTOKANA NA MADAI YAO HAPO JUU
PAMOJA NA MADAI MENGINE MENGI AMBAYO HAYAJAORODHESHWA
MAJINA YA WAFANYAKAZI WALIOGOMA NI HAYA YAFUATAYO
1. SEVERINUS MWIJAGE Jr – MTANGAZAJI
2. BEATRICE GERALD NANGAWE – MTANGAZAJI
3. EMMANUE MWAKALUKWA – MTANGAZAJI
4. JALACK ALLY – MTANGAZAJI
5. HAMIS ABTWAY (DJ HAAZU) – MTANGAZAJI, MZALISHA
VIPINDI NA DJ
6. BERTHA ISMAIL – RIPOTA
7. ONESMO LOY – RIPOTA
8. JOSEPH AMANI – MZALISHAJI WA VIPINDI
9. ALLY CHARO – MENEJA WA MASOKO
10. RODGERS I. NELSON – MHASIBU
11. WITNESS RAYMOND – MASOKO
12. HAPPYNESS ALPHONCE – MASOKO
No comments:
Post a Comment