Wanasayansi wagundua nyoka mwenye umbo kama ‘uume’




Wanasayansi nchini Brazil wamegundua aina ya nyoka vipofu wenye umbo kama uume wa binadamu.

Tuwie radhi kama picha hizi zitakuondolea hamu ya kula lakini huu ni uumbaji wa Mungu.

Nyoka hawa wa ajabu aina ya ‘atretochoana eiselti’ walipatikana kwenye bwawa la kuzalisha umeme ambapo wakandarasi walikuwa wakifanya ukarabati kwenye misitu ya Amazon.

Wana baiolojia waliwapata nyoka hawa wenye umbo la ajabu sita wenye urefu wa mita moja chini ya mto Madeira huko Rondonia, Brazil.

Nyoka huyo anaweza akawa na muonekano usiopendeza lakini huu ni ugunduzi unaovutia kwa wanayasansi wanaomini kuwa wanauhusiano na vyura.

Wanasayansi wamesema licha ya viumbe hao kuonekana kama nyoka lakini sio jamii ya reptilia.

Mara ya kwanza waligunduliwa America ya Kusini mwaka 1968.

No comments:

Post a Comment