Jana Club ya soka ya Azam ilitangaza kwamba Mchezaji wao Mrisho Ngasa tayari amepelekwa Simba kwa mkopo ambapo Simba walipewa sharti la kuhakikisha wanamlipa Ngasa mshahara wake kamili (TZsh 2,000,000) kwa mwezi pamoja na stahiki zake nyingine zote za kimkataba.
Sababu za kumpeleka Ngasa kwa mkopo ni kumuepusha na adhabu ambayo klabu ya Azam FC ingetoa kwa Ngasa kama angebaki Azam Fc, Pia iliwekwa wazi kwamba Azam haijamlazimisha Ngasa kwenda Simba kama inavyopotoshwa, Kama Ngasa anataka kuvunja mkataba wake au kama Yanga bado wanamhitaji basi waje na dola 50,000 na Azam FC itawauzia kwani licha ya kwamba amepelekwa kwa mkopo simba lakini Ngasa bado ni mali ya Azam FC.
Azam ilisema “Tunaomba kuweka msimamo wetu kuwa hatupo tayari kumlipa Ngasa na kuvunja mkataba wake na hatuna sababu ya kufanya hivyo. Kama Ngasa hataki kwenda tunakompeleka Azam FC inamruhusu kubakia klabuni na kutumikia adhabu, Lakini Ngasa na washauri wake waelewe kuwa akiamua kubaki Azam FC atakaa nje ya uwanja kwa muda wote uliosalia kwenye mkataba wake, kwani Azam FC haipotayari kumvisha jezi mchezaji anayefanya vitendo vya utovu wa nidhamu”
Azam ilisema kosa alilolifanya Ngasa ni kubusu na kuvaa jezi ya Yanga wakati bado ni mchezaji wa Azam hivyo ilionekana ni kitendo cha nidhamu mbovu na kuidhalilisha brand ya Azam.
No comments:
Post a Comment