Shettah aelezea sababu za Lady Jay dee kukataa kupiga nae collabo katika wimbo wake mpya 'Bonge la bwana'.

Shettah
Siku kadhaa zilizopita msanii aliefanya vizuri na nyimbo kadhaa ikiwemo 'Nidanganye' Shettah, alitangaza juu ya wimbo wake mpya aliopanga kumshirikisha binti machozi Lady jay dee.

Kupitia Power Jams ya EA radio, Shettah ameelezea mabadiliko yaliyojitokeza juu ya wimbo huo ambao imebidi amshirikishe Linah Sanga na sio Jide kama alivyotangaza awali. Shettah amesema hapo awali alikuwa ameshawasiliana na Lady Jay dee aliyemkubalia kufanya nae wimbo huo na Shettah alimpatia title ya wimbo ili aweze kujiandaa nayo. Mabadiliko yalikuja kujitokeza baada ya Jide kuiskia mistari ya Shettah ya wimbo huo kitu ambacho kilimsababisha kukataa kuimba katika wimbo huo kama walivyokuwa wamekubaliana mwanzo. 

"mwanzo alikuwa amekubali kabisa na nikampa title ya 'Bonge la bwana' lakini alipokuja kuiskia mistari akasema hakujua kama mimi nimeimba hicho nilichoimba so ni ngumu yeye kuimba sababu hafit kwenye idea hiyo maana hata kiumri yeye ni mkubwa kwangu, ila akasema labda niibadilishe kidogo idea kitu ambacho nimeona kitafanya na mimi nibadilike kuanzia mwanzo mpaka mwisho huku ngoma tayari iko poa. So nimeamua kuifanya na Linah na Jide kasema poa nifanye na mtu mwingine halafu yeye ntakuja kufanya nae wimbo mwingine" alisema Shettah.

Shettah anategemea kuuzindua wimbo wake huo mpya wa 'Bonge la bwana' pale Maisha club tarehe 25 mwezi huu wa November, na amewataja wasanii watakao mpa support katika show hiyo kuwa ni pamoja na Feruz, Jaffarai, Pasha, One, Stereo, Young Dee, Shilole na wengine. 

Wimbo huo umerekodiwa pale G-Records na video yake inatarajiwa kufanywa na Adam Juma wa Visual Lab Next Level.

Major Harris wa "The Deflonics" Afariki dunia akiwa na miaka 65.


Anaitwa Major Harris…aliyekuwa member wa kundi la muziki wa soul kutoka Philadelphia “The Delfonics” ameripotiwa kufariki dunia huko Richmond, Virginia.
Vyombo vya habari vya karibu vimeripoti kifo hicho kutokea ijumaa Nov 09 kutokana matatizo ya moyo aliyokuwa nayo muda mrefu na kushindwa kufanya kazi kwa mapafu ambako kulipelekea kukimbizwa hospitali na baadae kufariki dunia.
Kihistoria Major Harris alianza muziki long time..mwishoni mwa miaka ya 50’s na aliwahi kuwa member wa makundi kibao tu kama Charmers, Frankie Lymon’s Teenagers na Nat Turner’s Rebeillion kabla hajamalizia muziki wake The Delfonics mwanzoni mwa 1970’s ambapo walitengeneza hits kama “La-La (Means I Love You) and “Didn’t I (Blow Your Mind This Time)”.
Wasanii kibao wa HipHop wa mid era wame-sample ngoma kibao za The Deflonics…baadhi yao ni pamoja na Grand Puba “Very Special”, Ghostface Killah “Holla” & “R.A.G.U.” na Fugees “Ready or Not”..R.I.P Major Harris.

Sababu iliyofanya Steve RnB kufanya wimbo ambao sio RnB ' RnB'



Mkali wa R&B bongo aliyewahi kuingia kwenye top 5 ya wakali wa chorus TZ kwa mujibu wa uchambuzi uliofanywa na Leotainment, amefunguka kuhusu sababu zilizompelekea yeye kuachia wimbo aliomshirikisha Ommy Dimpoz ‘Radio’ ambao sio R&B na na hauna mahusiano ya karibu na R&B.
Katika interview aliyofanya na Leotainment, ‘The Tabasamu chorus Killer’ alisema sababu ambazo zilimpelekea yeye kuachia wimbo huo ni biashara tu na uamuzi wa kumshirikisha Ommy Dimpoz ni kwa sababu alitaka mashabiki Ommy Dimpoz wawe mashabiki wake pia.
“Unajua muziki sasa hivi yaani ni mpana sana, kwa hiyo kwa mimi nimeona kama ni nauwezo mkubwa sana wa kufanya nachoweza kufanya coz nilikuwa nahitaji pia mashabiki wa Ommy Dimpoz ambae ndiye niliyefanya nae kazi wawe pia mashabiki wa Steve R&B. So what I think kwamba mimi nilichofanya yani nimefanya biashara yaani bishara ya kimuziki ni vitu ambavyo vinaweza kufanyika pia kwenye game, kama ya industry ya muziki wetu unaweza kufanya kitu flani kwa ajili ya kuongeza mashabiki na kuonesha uwezo wako unaweza kufanya nini....” ni baadhi ya sentensi kibao alizofunguka Steve RnB.
Kuhusu issue ambayo wengi huwa wanazungumza kitaa kuwa the real R&B kwa bongo haiuzi kiivyo kama style nyingine na huenda ikwa ni sababu iliyopelekea Steve kuhamia hizi style za Nigeria na kudondosha ‘Radio’ na Ommy Dimpoz, alisema “sio kweli kiukweli nakataa coz mimi kilichonitambulisha ni R&B na sio muziki mwingine. Mi naweza kusema ni kubadilika tu.”
Steve aliwataja wasanii kwenye game Lady Jay dee na T.I.D ambao mwanzoni walikuwa wanafanya R&B lakini baadae wamebalika na kujichanganya pia na mitindo tofauti tofauti.
Kwa mujibu wa Steve R&B sasa hivi amehama management ya Zizzou entertainment na sasa yuko Combination entertainment ya Man walter ambayo ndiyo inafanya ngoma yake hii iliyotoka hivi karibuni, na pia ndiyo itakayosimamia project zake kwa sasa.
Steve R&B ni jina ambalo hutaacha kulitaja kama utaambiwa kutaja majina matano ya wasanii wanaofanya real R&B hapa Bongo na kusikika kupitia media kibao. Kwa kumbukumbu za haraka haraka Steve aliitwa R&B baada ya ku-kill ile chorus ya ‘Tabasamu’ aliyopewa shavu na Mr. Blue na baadae kuendelea kuua kwenye ngoma kibao za R&B ambazo zimempa heshima kubwa sana Bongo huku akiendelea kuzipendezesha chorus za wana Hip Hop pia.

Lord Eyez, wakili wake na weusi wazungumzia kesi inayomkabiri, ahaahidi kuwasapraiz fans wake


Lord Eyez (kulia) akiwa na wakili wake wakati wakiongea na waandishi wa habari

Mweusi toka A- City, Lord Eyez amekutana na waandishi wa habari akiwa na wakili wake ili kuzungumzia kesi inayomkabiri ya wizi wa vifaa vya gari ambayo ili-make headlines sana siku kadhaa zilizopita.
Lord eyez amesema yeye kwa sasa anaiachia mahakama ambayo ndiyo itaweza kuchukua maamuzi ya kisheria kama yeye alihusika ama hakuhusika katika wizi huo wa vifaa vya gari.
Wakili wa msanii huyo anayejulikana kwa jina la Peter Kibatala amesema kesi hii imefanya mpaka Lord Eyez kuonekana kwamba yeye ndiye mhusika wa wizi wa vifaa hivyo lakini kwa sasa hivi wanaiachia kwanza mahakama ndiyo itakayoweza kuchukua uamuzi sahihi kuhusiana na kesi hiyo.
Hizi kauli za mweusi huyu na wakili wake zinaonekana zimepimwa na ruler ya kisheria kwa sababu ni kosa kisheria kujadili kesi ambayo iko mahakamani (commenting on a pending case).
Weusi nao walisema ‘neno’ kuhusu tuhuma zinazomkabili member huyo na kwamba tukio hili limewaathili hasa pale wanapokutana na watu mbalimbali na kusikia story toka kwa watu kwamba wote watakuwa wanahusika katika tukio hilo wakati ni story ambazo sio za kweli.
Kesi hiyo inatarajiwa kusomwa katika mahakama ya mwanzo jijini Dar es Salaam tarehe 13, 14 na 15 mwezi huu wa Novemba.
Hata hivyo the N2N soldier amesema kwa sasa anachotaka kufanya ni kudondonsha ngoma yake mpya kali ambayo anataka kufanya ‘surprise’ kwa mashabiki wake katika industry ya muziki wa Bongo.
Lord eyez alituhumiwa na msanii mwenzake Ommy Dimpoz kuwa alishirikiana na wenzake kumuibia vifaa vya gari lake na tuhuma hizo nzito ambazo ni pigo kwa kundi la weusi kiujumla zilipelekea Lord Eyez kukamatwa na kushikiliwa kwa na jeshi la polisi kwa siku kadhaa na baadae kufunguliwa kesi mahakamani ambapo alipewa dhamana.

Chris Brown aweka wazi uhusiano wake na Rihanna, “ sitaki kuharakisha kitu, kuweka pete yeyote kwenye kidole cha mtu yeyote...”



The R&B star amefunguka vizuri zaidi kuhusu uhusiano wake na ex girlfriend wake Rihanna baada ya kuonekana pamoja mara kwa mara bila kutoa tamko rasmi linalozungumzia uhusiano wa wawili hao ukiacha mbali ile video aliyoiachia baada ya kuachana na Karrueche Tran na kukiri kuwa bado anawapenda wote.

The ‘don’t work me up’ hit maker amesema katika interview, “ni mimi kuwa mkweli na nafsi yangu. Mimi na Rihanna tuna historia, na mimi na yeye tutaendelea kuwa best friends, na tunafanyia kazi mahusiano yetu sasa.” Mkali huyo anajua kabisa kuwa watu wanasema mengi kuhusu mahusiano yao ambayo hayaeleweki vizuri mbele za watu, ni marafiki wa aina gani ama ni wapenzi wa aina gani hawa.

Kuhusu hilo akafunguka, “nadhani kila mtu anaguswa na hii situation ya zamani, bado ni hali ya hatari, kwa sababu ni yale tunayo-deal nayo leo na ndio maana nafanya Jenesse Center ambayo inaonesha kuwa domestic Violence sio sawa. Lakini kuhusu maisha yetu, nadhani watu wanatakiwa kuyapa nafasi, sio tu kuyapa nafasi, shut the hell up! Mwisho wa siku, maoni yoyote yale hayawezi kubadili chochote ninachofanya.”

Ingawa anafeeling kwa Rihanna, Breezy amesema haoni dalili za ndoa katika maisha yao ya hivi karibuni,na kwa nini aliamua kuachia video ambayo aliongelea kuhusu kuwapenda wanawake wawili.

“Ninapojisikia hali flani, iwe ni ya muziki ama emotion, najisikia ni vizuri kushare na watu, kwa sababu ni experience na fundisho katika maisha.”

Na kuhusu kuwepo na wazo la ndoa alifunguka, “sijaribu kuharakisha mambo, kuweka pete yeyote kwenye kidole cha mtu yeyote au kudanganya mtu yeyote. Ni bora niwe mkweli kabisa.”

T-Boz wa TLC asema Nick Minaj akafanye Porn sio kuwa jaji “How the hell is she gon’ tell me what I should be doing when her as* can’t even sing”


T-boz
Member wa TLC T-Boz amemvaa tena rapper wa Young Money Nicki Minaj ambae ni jaji wa mashindano ya kuimba yenye lengo la kuibua vipaji ‘American Idol’. T-Boys hakubaliani kabisa na kitendo cha rapper huyo wa kike kuwa jaji wa mashindano ya kuimba wakati yeye sio mwimbaji na kwa maoni yake kitu ambacho anaweza kufanya hata bila kuwa na kipaji ni Porn.
Katika interview kwenye ‘this is Max in London’ mwimbaji huyo wa kike wa kundi la TLC alifunguka kwa madaha, “kwa sababu tu unaonekana kwenye mzunguko wa TV, boning and sucking p*enises’, sio kipaji, honey labda kwenye soko la Porn, lakini sio hapa (kwenye muziki), tunaburudisha. Siheshimu nusu ya watu ambao nimewaona hivi karibuni. Ataniambiaje nini nachotakiwa kufanya wakati hawezi hata kuimba?
“Kwa nini yuko pale? Halafu...sasa wana rapper ambae hata haimbi na anajaji? So, hii inaonekana imeegemea kwenye umaarufu nahisi., namaanisha, kwa kile anachopata kila mmoja wao. Chukua mkwanja wako, honey. Nachosema ni kwamba sitaangalia show yenu tena.” Ndo maoni ya T-Boz kuhusu nafasi ya ujaji wa Nicki Minaj kwenye mashindano ya kuimba “American Idol”.
Hata hivyo baada ya maoni yake kutolewa kwenye media mbali mbali T-Boz aliamua kutumia account yake ya twitter kuweka kulezea zaidi kile alichosema. Hizi ni baadhi ya tweet zake:
“Im laughing at y’ll guess u told me huh lol My whole comment wasn’t about chick but some of the guest appearances & not Brittney at all” ilikuwa tweet yake ya November 8.
“& it’s not a diss these shows are based on popularity & bringing in the viewers & bringing their umbers up not based on picking talent lol.”
Nicki Minaj ni moja kati ya majaji wanne wa American Idol na yeye pekee ndiye rapper na tangu achaguliwe kuungana na majaji wenzake ameshakwaruzana na Mariah Carey ambae ni jaji mwenzake kwenye shindano hilo. Minaj ameachia reality show yake ‘My truth’ikiwa na vipande vinavyoelezea uwepo wake kwenye shindano hilo kama jaji.

Robert Pattinson Dodges Kristen Stewart Relationship Rumors










After months of speculation of whether they are or aren't back together, "Twilight Saga: Breaking Dawn -- Part 2" costars Robert Pattinson and Kristen Stewart are speaking out on the status of their relationship, whether they want to or not.
On Wednesday, Stewart stopped by the "Today" show to promote the final "Twilight" installment and was asked by co-host Savannah Guthrie if she and Pattinson had reconciled.


"I'm just going to let people watch whatever little movie they would like to think our lives are, and keep them guessing I always say," Stewart said.
On Thursday (November 8), it was Pattinson's turn in the hot seat when he sat down with Guthrie. She asked Pattinson if he had heard Stewart's answer to the question fans have been dying to know.
"Keep 'em guessing?" he repeated after Guthrie informed him of KStew's response. "I want to ask, because we get asked it all the time, everyone always asks, like for four years. Who is actually asking? Is it in your contract?" he asked Guthrie.
"Yes, it's in the fine print," she said laughing.

This was the first time that Pattinson has been asked or spoken about the status of his relationship with Stewart, and he was clearly taken aback. Guthrie, not backing down, then followed up asking if his success with the "Twilight" is a "high price to pay" since "it is personal" for him now.
"Doesn't have to be," Pattinson said. "It only becomes personal if you answer it. I could sit here and talk nonsense about paper hats and stuff, getting old, needing a nap."
Stewart and Pattinson first met on the set of the first "Twilight" film back in 2008 and there has been speculation regarding their relationship ever since, but the two never publicly addressed their romance until Stewart issued a public statement apologizing to Pattinson for her "momentary indiscretion" after photos were released of her getting cozy with her "Snow White and the Huntsman" director Rupert Sanders in July.
Last week, Pattinson and Stewart sat down with MTV News during "MTV First: 'Twilight: Breaking Dawn - Part 2,' " where Pattinson and Stewart both revealed which "Twilight" scene they would want to reshoot: the first kiss scene.
"It's hard though. That was a hard scene," Pattinson said. "That was the audition scene as well. But, it's like in order... I don't know. It's just a difficult one."