Kanye West hakuhudhuria tuzo za Grammy, kisa alimpeleka Kim Kardashian mapumzikoni Brazil, walikaa hotel moja na Will Smith.




Kanye West alilazimika kutohudhuria tuzo kubwa na zenye heshima sana duniani ‘Tuzo za Grammy’ zilizofanyika jumapili February 10, sababu kubwa ikiwa ni kumfurahisha girlfriend wake mwenye ujauzito Kim Kardashian.

Boss wa G.O.O.D music alimpeleka Kim Kardashian Brazil kwa ajili ya mapumziko ambapo waliingia hapo tangu ijumaa, na wakaanza kuonekana wakipiga misele na kupiga picha maeneo ya kitalii ya Rio de Janeiro na maeneo mengine wakiwa katika mapozi ya mahaba.


Yeezy na K.K walionekana wakipiga picha katika hotel waliofikia maenoa hayo ya Rio de Janeiro ambapo rapper Will Smith pia alikuwa ameweka kambi, kitendo cha celebs hao watatu kuwa pamoja katika hotel hiyo kiliwafanya mashabiki kibao kufika hotelini hapo na kushangilia kwa nguvu mara kwa mara, na kwa mujibu wa Kim Kardashian wengi walikuwa wanamshangilia Will Smith.

Kim aliweza kuchukua clip ya video na kushare kwenye Keek page yake na kuandika, “Will Smith gets the crowd going”. Aliweka clips nyingine mbili zinazomuonesha akiwa kaweka pozi na nyuma kuna umati mkubwa wa fans.



Japokuwa hakuhudhuria kwenye utoaji wa tuzo hizo Yeezy alinyakuwa tuzo tatu, na jumatatu Kim Kardashian alitweet, “Awww just waking up in Brazil, seeing Kanye won 3 Grammy’s last night!!! That makes a total of 21!!! That’s just so insane! Soooo proud!!!”


Kwa mujibu wa mtandao wa Usatoday, Kanye West alisema tangu mwezi December kuwa hatahudhuria utoaji wa tuzo za Grammy mwaka huu.


Ilimbidi Jay-Z apokee tuzo akimuwakilisha swaiba wake Kanye, wimbo wao N*ggas in Paris ulishinda tuzo mbili ‘Best rap performance na Best rap song.” Na Kanye aliichua tuzo nyingine katika wimbo wa kushirikiana ‘No Church in the Wild akiwa na Jay-Z, wakiwashirikisha Frank Ocean na The-Dream.”

No comments:

Post a Comment