Mkali wa michano aliyetisha sana mwaka 2012 Stamina a.k.a
Kabwela amefunguka kuhusu mipango mbalimbali aliyokuwa nayo mwaka jana na hatua
aliyopiga katika muziki wake na show 61 alizopiga mwaka huo. Kuhusu show
alizopiga mwaka jana show ambayo hataisahau ni show ya Fiesta Dar ambayo
alifunika vibaya na kwamba hakuwahi kufanya show kama ile.
'Kabwela' hitmaker mwenye misemo kama kamusi amefunguka
katika interview aliyofanya na Lucas Maziku wa Radio SAUT Fm ya Mwanza, kuwa
mwaka 2012 alipanga kufanya kazi na marehemu Steven Kanumba, na walipanga
kufanya movie ya wimbo wake wa "Kabwela" lakini bahati mbaya
alifariki kabla hawajakamilisha mpango wao huo, lakini mwaka huu ataifanya
movie hiyo.
Lakini pia Marehemu Sharomilionea alipanga kumpa shavu
kwenye wimbo wake mmoja ambao Sharo alipanga kumuimbia mama yake, na mipango
ilikuwa tayari lakini Sharo alisema itabidi asafiri akirudi watafanya wimbo huo
pale C9, na bahati mbaya hakurudi baada baada ya kupata ajali na kufariki.
"Hata kwenye ule
wimbo tulifanya wa kumuenzi nilisema, alisema kwamba akisafiri akirudi, kuna
ngoma tutafanya alikuwa anamuimbia mama yake, nikikuwa mimi niko featured,
alilkuwa kanishirikisha, ikuwa inataka kufanyika pale kwa C9 lakini na yenyewe
pia Mungu kampenda zaidi, kwa hiyo ni vitu ambavyo vinaniuma sana."
Kuhusu mafanikio aliyoyapata ni kwamba alifikia level nzuri
sana alihama kutoka kwao na kupanga ili aishi maisha yake mwenyewe, hakuwa na uwezo
wa kwenda chuo kwa sababu ya mkwanja lakini sasa hivi ameshakichanga na yuko
tayari kuingia chuo mwaka huu. Akicheka kwa kwa utani kidogo alisema hadi sasa
anafurahi kuona anaendesha gari lake mwenyewe.
Stamina amesema ameweza pia kuzifikia sehemu ya ndoto yake,
na kwamba ameweza kufanya kazi na msanii anaemkubali sana Fareed Kubanda a.k.a
Fid Q, na kwamba amefanya nae ngoma yake mpya inayoitwa "Toleo
Jipya". Sio hayo tu lakini pia ngoma imefanywa kwa producer of his dream
P-Funky Majani.
Kuhusu Kutosikika kwa muda kwa kundi la Mtu Chee linaloundwa
na yeye, Country Boy na Young D, amesema mgao wa mapato ulileta shida
ukizingatia wao hawakuwa na meneja na Young D ana management yake tayari,
meneja wa Young D alikuwa anataka asilimia nyingi zaidi ya mgao na sio mgao
ulio sawa kwa member wote kitu ambacho kilileta utata na kulinyamazisha kwa
muda kundi hilo, lakini sasa wameshakubaliana na management ya Young D na
wanarudi tena hewani kama Mtu Chee.
Pamoja na mafanikio aliyoyapata mwaka jana, bado Stamina anaona
kama haijawa poa kiivyo na mwaka huu ndio utakuwa mwaka wa kuoneshana ubaya.
"Nahisi kama
mwaka 2012 sikufanya kitu lakini mwaka 2013 ndo tutaoneshana ubaya, kwa sababu
kuna project nyingi sana zinakuja ukiacha mbali hiyo ngoma yangu na Fid, video
yake...halafu mwisho wa mwezi wa kwanza ntadrop album yangu ya kwanza
uswahilini, iko tayari inaitwa "ALISEMA".
No comments:
Post a Comment