Amber Rose ataja jinsia ya mtoto wao mtarajiwa ‘bila kukusudia’! Alidai ndoa kabla ya kujifungua.



Amber Rose ambae ni girlfriend wa Rapper Wiz Khalifa ameandika tweet kwa followers wake million 1.4 iliyotaja jinsia ya mtoto wao wanaemtarajia.  lakini katika tweet hiyo anaonesha kama hakuwa na plan ya kutaja jinsia ya mtoto huyo ila ni kama ameitaja accidentally,wanatarajia mtoto wa kiume.
Lakini hii inawezekana aliamua tu kwa sababu ameandika katika tweet moja hiyo hiyo message inayotaja jinsia ya mtoto wao mtarajiwa na hapo hapo anashtuka kama kataja bila kujua.
Tweet yake ya jumapili ilikuwa inasomeka “My friend Maria bought our Lil Boy this Slash onesie….Oops did I say Lil Boy???
Hata hivyo Media za U.S.A zimefatilia sana kujua jinsia ya mtoto mtarajiwa wa mastaa hawa, na wiki iliyopita gossip sites zilitangaza jinsia ya mtoto wao na kusisitiza kuwa wamefatilia na wamepata uhakika kuwa ni mtoto wa kiume na hii ni kutokana na shopping wanazofanya mastaa hawa ambapo vitu vinavyonunuliwa kwa ajili ya maandalizi ya mtoto wao inaonesha wazi kuwa ni mtoto wa kiume, hasa vitu vya rangi ya blue.

Lakini hata ukifatilia statement za Wiz Khalifa mwenyewe huwa anataja kiwakilishi ‘HE’ akiwa anamzungumzia mtoto wao japo hajawahi kusema kuwa ni mtoto wa kiume lakini hii pia ilikuwa inamaana. Mwezi August alimwambia rapper Colloway “You’re going to teach him how to rap.”

Hivi karibuni pia Amber Rose alipokuwa anazungumzia mipango yao ya kumpokea mtoto wao katika maisha yao alisema wanapanga kuoana kwanza kabla hajajifungua mtoto.
“Nah, hakuna tarehe iliyopangwa bado. Lakini tunaweza kupata license na kufunga ndoa kabla mtoto hajazaliwa, na tutafanya sherehe baadae kwa sababu italeta maana kwa mtoto kuzaliwa katika wedding na zaidi ya kuwa katika hii hali ya ujauzito tu. Watu wengine wanaharakisha na kufanya. Lakini njia zote zinawezekana” alisema Amber Rose ambae ni Ex girlfriend wa Kanye aliyezama kwenye bahari ya penzi la rapper Wiz Khalifa.

Hatimaye Justine Timberlake na Jessica Biel wafunga ndoa.


Wanandoa Timberlake & Jessica Biel

Safari ya mapenzi kati ya mkali wa R&B Justine Timberlake na muigizaji nyota Jessica Biel waliyoianza mwaka 2007 sasa imefika pazuri baada ya wawili hao kufunga ndoa na kuhalalisha mahusiano yao kama mke na mme.
Ndoa hiyo imefugwa Borgo Egnazia Resort nchini Italy katika jiji la Fasano. Mastaa hao waliwekeana ahadi za kuishi pamoja katika kila hali na kushuhudiwa na familia zao pamoja na marafiki.
Wanandoa hao wapya walionekana kuifurahia sana siku hii ya ndoa yao na kwa pamoja walisikika wakiwaambiwa watu “It’s great to be Married.”
Timbaland producer na mwanamuziki ambae ni swaiba wa Timberlake na mtu wanaeshirikiana katika muziki ni moja kati ya marafiki wa karibu waliokuwepo ukumbini.
Hakuna siku nzuri kama hii hasa kufunga ndoa na mtu ambae ulimpenda kwa siku nyingi na kuwa na ndoto ya kufunga nae ndoa siku moja na sasa ndoto hiyo imekuwa kweli, na hii ndiyo sababu ilimfanya Timbalake na mkewe Jessica kusema kwa pamoja “It’s great to be married.”

Rick Ross & Gucci Mane wamchana Young Jeezy ,wamtaka awape heshima.


Nitaurudia msemo uliozoeleka kuwa ‘adui wa adui yako ni rafiki yako kwa muda huo’ na hiki ndicho kinaonekana, kati ya vitu vinavyowaweka pamoja Gucci Man na Rosay sasa hivi ni ‘kila mmoja anabeef na Young Jeezy’.

Siku chache baada ya Gucci Mane kutoa wimbo aliupa jina la ‘Truth’ ikiwa ni diss moja kwa moja kwa Young Jeezy, sasa Rick Ross ameamua kumuongezea nguvu na kwa pamoja wametoa ngoma ya kumdiss Young Jeezy wakitaka awape heshima yao na ngoma hiyo wameibatiza jina “Respect”.
Katika track hiyo kuna mashairi ya moja kwa moja kwenda kwa Young Jeezy, ambapo Gucci alichana “Aint no way in hell I’ma let you desrepect me… Mad I’m fu**ng ur wifey” na Rick Rosay kiongozi wa May Back Music Group akaingia na verse yenye baadhi ya mistari kama “I push a button and them killers comin’/ Disrespect me, ni**as get nothing’.
Rosay na Young Jeezy wanabeef ambalo lilionekana waziwazi wakati wa kurekodi matukio ya BET Hip-Hop awards 2012 ambapo walifikia hatua ya kusukumana wakiwa back stage.
Mwenyewe Young Jeezy alizungumzia beef kati yake na Gucci Man mwanzoni kabisa mwa mwezi huu na akasema “ Najisikia kama kila mtu anamjua yule kijana, hakuna anaemchukulia seriously. Ana Ice Cream Cone usoni. Wanasema narudi nyuma. Mimi naenda mbele. And it’s crazy kwa sababu watakuita kwenye wimbo wao. Na usipotokea kwenye huo wimbo wao, hicho ndicho kinachotokea.”

Mastaa wampongeza Drake kwa kuhitimu High School.


Drake

Kweli elimu haina ustaa na inaweza kuwa kweli kabisa tena 99.9% kuwa ni ufunguo wa maisha, pamoja na kuwa na jina kubwa sana katika ulimwengu wa muziki na kuingiza mkwanja mrefu sana, bado Drake hakukubali kupitwa na elimu, na kwa kukomaa na vyote hivi karibuni amehitimu high school na kuongeza CV ya taaluma.
Kikubwa zaidi ni kwamba Drake ameweka hadharani alama alizopata, ambapo amesema amepata 97% kwenye mtihani wa mwisho na 88% kwenye course. hizi ni alama nzuri, kweli Drake sio kilaza.
Baada Rapper huyo kutangaza hadharani kuwa amehitimu masomo ya high school watu mbali mbali wakiwemo mastaa wa Hip Hop na mastaa wa Hollywood wamempongeza, na wakati huo huo wapo watu wengi ambao wameshangaa kwa sababu hawakujua kama anasoma.
hongera zako Drake, na huu utakuwa mfano mzuri wa kuigwa na baadhi ya wasanii hasa wa bongo, wanaoacha shule eti kwa sababu ya muziki.

Hiki ndicho Bonta angependa kitokee kwa makundi ya Hip Hop Tanzania, kuhusu alichosema Nikki Mbishi “No Comment”.


Bonta

Bonta a.k.a Maarifa hivi karibuni ameachia wimbo wake unaoenda kwa jina la ‘Tukutane Maktaba’ ambao umesababisha maoni mbali mbali kutoka kwa watu hasa kupitia mitandao ya kijamii kama facebook, wengi wakimpa big up kwa kazi yake, lakini pia alipata criticism toka kwa Nikki Mbishi wa Tamaduni Music ambae amekuwa akiandika status kuwamcriticise Bonta na baadhi Weusi.
Mweusi toka katika kundi la River Camp Soldiers alifanya interview na Josefly mtangazaji wa victoria fm iliyoko Musoma, kupitia kipindi cha Over drive.
The river camp doctor alifunguka mengi kuhusu ‘tukutane Maktaba’, kisha mtangazaji huyo aliuliza “baada ya kuachia ngoma yako watu wengi walionekana kuipokea vizuri kupitia mitandao mbali mbali ya kijamii na blogs mbalimbali, lakini kuna criticism, unamfahamu jamaa mmoja anaitwa Nikki Mbishi?” Bonta alijibu “ah, hiyo no comment, hilo siwezi  kuzungumzia kwa sababu kila mtu ana uhuru wa kuongea kitu chochote anachotaka kwenye nchi yetu, kwa hiyo no comment kwa hilo mtu wangu.”
Na kuhusu kile anachotamani kitokee kati ya makundi yote ya hip hop Tanzania ambacho kingemfanya aone kakundi yamepiga hatua Tanzania, alifunguka, “mi natamani kila kundi lifanye muziki wake na kila kundi litumie miguu yake kutembea kufika pale linapotamani na lisitumie mgongo wa kundi lingine, lisitumie midomo yao vibaya wala lisitumie freedom of speech vibaya, kila mtu afanye kazi yake na kila aheshimu kazi ya mtu, au sio, usitumie effort ya mtu ambayo ameshatengeneza ili upate negative publicity, at the  end of the day unajua mashabiki wako ndio mashabiki wangu, mashabiki wangu wataendelea kuwa mashabiki wangu na mashabiki wako wachache watakuja kwangu.”

Mikasa yamuandama Justine Bieber,Baada ya kuibiwa laptop kwenye show, sasa adondoka kwenye ngazi wakati anaperform.


Mikasa yamuandama Justine Bieber,Baada ya kuibiwa laptop kwenye show, sasa adondoka kwenye ngazi wakati anaperform.

Mikasa inazidi kuiandama tour ya ‘Believe’ ya Justine Bieber ikiwa ni siku chache baada ya kuibiwa laptop yake akiwa stejini huko Arizona Washington, sasa amepata mkasa mwingine baada ya kuanguka alipokuwa anaperform huko Saskatchewan Canada usiku wa October 17.

Bieber alikuwa anakaribia mwishoni kabisa kumalizia wimbo wake wa Beautiful aliokuwa anaupiga na Carly Rae Jepsen, msichana huyo alishuka kwenye ngazi za steji akiwa na Justine Bieber, lakini kwa bahati mbaya Bieber alimiss step moja kwenye ngazi akakosa balance na akaanguka.
Baada ya tukio hilo immediately Jepsen alimshika mkono Bieber na kumuinua, na mkali huyo aliweza kusimama na kuendelea kumalizia perfomance yake kama vile hakuna kitu kam hicho kilichotokea pale.
Mkali huyo ambae ni boyfriend wa Selena Gomez anatarajia kuendelea na tour yake ‘Believe’ hadi mwakani. na ratiba yake inaonesha kuwa baada ya hiyo show ya Saskatchewan ataelekea Winnepeg na Minneapolis kati ya October 18-20. na baada ya hapo anatarahji kuingia Ulaya around February 2013.