Goldie na Prezzo.
Ni taarifa ambayo kila aliekua karibu na Goldie kwenye
page zake za facebook na twitter inakua ngumu kuamini, taarifa rasmi zimeripoti
kwamba Goldie ambae ni mwakilishi wa Nigeria kwenye BBA 2012 AMEFARIKI muda
mfupi tu baada ya kuwasili Lagos Nigeria akitokea Marekani ambapo bado chanzo
cha kifo chake hakijajulikana.
Mmoja wa wasaidizi wake amethibitisha kifo cha Goldie
kupitia page ya twitter ya Goldi kwa kusema ni kweli msanii huyo amefariki
dunia usiku wa february 14 2013 muda mfupi tu baada ya kuwasili Lagos Nigeria,
hali yake ya afya ilibadilika ghafla ikabidi apelekwe hospitali ambako
hakuchukua muda mrefu akafariki dunia.
Taarifa nyingine nilizozipata kutoka kwa mtu wake wa
karibu wanaeshirikiana kimuziki zimeeleza kwamba mpenzi wake Goldie ambae ni
Msanii wa Kenya CMB Prezzo ametua Nigeria usiku huu muda mfupi uliopita kwa
ajili ya kuendeleza mipango aliyokua nayo na Goldie ikiwemo kutengeneza show ya
TV.
Prezzo alitakiwa kushiriki katika TV show ambayo yeye na
Goldie wangekua moja ya wahusika wakuu ambapo mpango ulikua baada ya mwezi
mmoja Goldie na Prezzo wangekuja Tanzania, Uganda na Kenya kwa ajili ya
kujitangaza na kuipromote single mpya ya Goldie ya ‘Skibobo’ aliyofanya na Ay.
Huyu
Deji ni mtangazaji wa Radio huko Nigeria ambae Goldie ndio
aliniunganisha nae, muda mfupi baada ya kupata taarifa za Goldie
ilibini nimtumie msg ili kujua kama ni kweli, na majibu yake ndio hayo
hapo juu.
Kwenye Exclusive interview na millardayo.com october
19 2012 alisema alikua na mpango wa kwenda Marekani kurekodi kolabo yake na
mastaa wawili wa muziki ambao ni Keri Hilson na Trey Songs ambao tayari mipango
ilikua tayari na kilichobaki ilikua ni makubaliano ya mwisho mwisho tu.
Marehemu Goldie kwenye interview na Millard Ayo wakati alipokuja Tanzania kurekodi single yake ya ‘Skibobo’ na Ay.
.
No comments:
Post a Comment